Simba Sports Club wameanza rasmi mazungumzo ya kina na aliyekuwa nyota wa Singida Black Stars, Antony Tra Bi Tra kwa lengo la kumsajili kama Mchezaji Huru (Free Agent) kuelekea dirisha dogo la usajili.
Antony Tra Bi Tra ni miongoni mwa viungo bora waliowahi kuichezea Singida Black Stars na amekuwa akifuatiliwa na Simba SC kwa muda mrefu, hata kabla ya kuwasili Singida. Kuvunjwa kwa mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote kunawapa Simba nafasi ya dhahabu kunasa saini yake bila gharama ya uhamisho.
Chanzo cha karibu na klabu kinadai Simba wanahitaji haraka kiungo mwenye uzoefu wa kimataifa kuongeza ushindani wa kikosi kuelekea mechi nzito za ligi na michuano ya kimataifa.
Hatua za mwisho za makubaliano zinatarajiwa kukamilika muda wowote kuanzia sasa.
