Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2026

Simba haooo Zanzibar

Kikosi cha Simba SC kimewasili Visiwani Zanzibar tayari kwa kushiriki mashindano ya Mapinduzi Cup ambayo yanaendelea visiwani huko. . Kwa mjibu wa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Bi Zubeda ni kwamba Klabu hiyo imepania kubeba taji hilo ili kurudisha heshima iliyopotea kwa miaka kadhaa

Alichoandika Dickson Job

Mwaka 2025 umekua Mwaka Bora sana kwangu Binafsi. Nimevaa jezi ya Taifa Stars kwa fahari kubwa, nikapigania bendera ya Tanzania kwa damu, jasho na moyo wote na kuwa sehemu ya historia ya kufuzu Hatua ya 16 Bora AFCON na Robo Fainali CHAN kwa mara ya kwanza tangu Taifa letu lipate Uhuru. Kwa Wananchi wenzangu Yanga tumepigana hadi mwisho, tukatengeneza historia kwa kutwaa Ligi Kuu, Kombe la FA na Ngao ya Jamii. Kila jasho langu uwanjani mwaka huu lilikuwa ahadi kwa mashabiki, kila ushindi ulikuwa sauti yenu Wananchi. Mafanikio ya 2025 siyachukulii kama mwisho, Ni deni la kunyoosha zaidi 2026. Kwaheri 2025 ya Historia, Heri ya Mwaka Mpya Tanzania 2026 

GAMONDI APEWE MKATABA WA KUDUMU KUNOA STARS YA AFCON 2027

Na Prince Hoza Matua NAWATAKIA kheri ya mwaka mpya wa 2026 na pia nawapa pole wale wote ambao walipoteza ndugu zao mwaka jana, lakini wengine wameuona mwaka mpya ila hawapo sawa kiafya, mwenyezi Mungu awape uzima na kurejea kwenye utimamu wa afya kusudi tulijenge vema taifa hili la Tanzania na dunia kwa ujumla. Bila shaka Watanzania tumeingia mwaka mpya wa 2026 tukiwa na furaha tele kufuatia timu yetu ya taifa, Taifa Stars kufuzu hatua ya 16 bora ya AFCON inayofanyika nchini Morocco. Shukrani kubwa ziwaendee wachezaji, benchi la ufundi la timu hiyo na viongozi wa Shirikisho la soka nchini, TFF kwa kufanikisha timu hiyo inaandika rekodi ya mara ya kwanza kufika hatua hiyo. Lakini kubwa ni kwa kaimu kocha mkuu wa timu hiyo Miguel Angel Gamondi raia wa Argentina ambaye uwepo wapo umesaidia timu hiyo kufika hapo, nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawapongeza makocha wengine waliofanya vizuri aliwemo Hemed Morocco ambaye alikuwa kocha mkuu wa timu hiyo. Morocco akisaidiana na Juma Mgunda na...