Wachezaji wa timu ya Simba SC ambayo kesho jioni itashuka uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kumemyana na Esperance ya Tunisia mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika.
Wachezaji wa timu hiyo walionekana wakifanya mazoezi kwa bidii wakisimamiwa na makocha wao wakiongozwa na mkuu Steve Barker.
Kwa vyovyote tusubirie soka litakalotolewa na wachezaji hao ambao wameonekana kuwa na morali ya hali ya juu na kupania mchezo huo wakitaka ushindi wa kwanza.














