Yanga Princess imeendelea kuifukuzia Simba Queens katika msimamo wa Ligi Kuu ya wanawake Tanzania bara, baada ya leo kuifunga Bunda Queens mabao 3-1 uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
Magoli ya Yanga Princess yamefungwa na Jeannine Mukandayisenga aliyefunga mabao mawili na Aisha Djafar wakati bao la Bunda Queens limefungwa na Kulwa Rocket.
Yanga Princess anamaliza raundi ya kwanza na ushindi mnono ugenini huku akiendelea kuwa nafasi ya pili chini ya Simba Queens.
Bunda Queens wameganda pale pale wanaruhusu vipigo nyumbani mfululizo.
