Golikipa wa Nigeria na klabu ya Chippa United ya South Afrika Stanley Nwabali amesema wachezaji wengi wa Afrika Magharibi huhamia Ligi ya Afrika Kusini kwa sababu inalipa vizuri na iko kwenye kiwango cha juu.
Kwa mujibu wake anasema Ligi ya Afrika Kusini na Morocco ni bora kuliko ligi nyingi za Afrika Magharibi.
Ndiyo maana wachezaji wa ligi hizo hawana presha ya kukimbilia Ulaya, kwa sababu tayari wanapata mazingira mazuri na malipo bora.
