Harouna Kahena maarufu kama Inspector Haroun a k a Babu msanii wa muziki wa kizazi kipya anayeunda kundi la Gangwe Mob ambapo miaka ya 2001 lilitamba sana kwa nyimbo zake za Mtoto wa Geti kali na nyinginezo.
Inspector Haroun ndiye aliyeasisi jina la Wekundu wa Msimbazi ambapo klabu ya Simba SC yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi ikaamua ilitumie kuwa na miongoni mwa majina yake ya utani.
Jina hilo, Inspector Haroun aliliimba katika wimbo wake uitwao 'Yanini bye bye " alioutoa mwaka 2002, na kuanzia hapo Simba SC ikaamua kujiita Wekundu wa Msimbazi.
Inspector Haroun aliamua kuiita noti ya elfu kumi, (10,000) iliyokuwa ya rangi ya bluu ambapo wakati huo msanii Mr Blue alijitokeza kutokana na noti hiyo, Harouna yeye akaiita elfu kumi mpya yenye rangi nyekundu ambapo akaiita wekundu wa Msimbazi, akisema "Na sasa sio bluu bluu tena ni wekundu wa Msimbazi ", na hapo ndipo Simba walipopata fulsa ya kujiita Wekundu wa Msimbazi.
KWAHIYO INSPECTOR HAROUN NDIYO MUASISI WA JINA LA WEKUNDU WA MSIMBAZI KWA SIMBA SC.

