Jeannine Mukandayisenga amevunja rekodi yake yeye mwenyewe aliyoiweka msimu pita akifunga mabao 13 kumbuka alicheza mzunguko mmoja tu aliingia Yanga dirisha kubwa la usajili.
Jeannine Mukandayisenga alifunga mabao 13 ya ligi wakati pia akifunga mabao matatu (3) kwenye michuano ya Samia Cup akimzidi Neema Poul aliyefunga magoli 12 kwa sasa yupo Fountain baada ya kuondoka Yanga.
Msimu huu ligi pekee amefunga mabao 16 katika michezo 11 ya nusu msimu
Ni wachezaji wawili tu wakigeni hadi sasa ambao wamefanikiwa kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania kwa misimu miwili tofauti mfululizo.
Jentrix Shikangwa (kutoka Kenya) na Asha Djafari (kutoka Burundi) wote walitwaa wakiwa Simba Queens.
2019/2020 – Fatuma Mustapha (JKT Queens): mabao 33 Mzawa.
2020/2021 – Aisha Masaka (Yanga Princess): mabao 35 Mzawa.
2021/2022 – Asha Djafari (Simba Queens): mabao 26
2022/2023 – Jentrix Shikangwa (Simba Queens): mabao 17
2023/2024 – Aisha Mnunka (Simba Queens): mabao 20 Mzawa.
2024-2025 -- Stumai Abdallah (Jkt Queens) : Mabao 27 Mzawa.
