NADIR Haroub Canavaro, ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa Tanzania nafasi yake Kiwanjani Ilikuwa ni Beki wa Kati (Center-defender) aliyezaliwa tarehe 10 Februari 1982, huko Michenzani, Zanzibar.
Nadir Alikuwa mchezaji mwenye umaarufu mkubwa sana nchini Tanzania, aliichezea Young Africans SC kwa miaka mingi Takribani miaka 12, ambapo alivaa jezi namba 23 na kuwa nahodha (captain) wa timu hiyo na pia ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars). Mbali na Yanga Sc, Nadir alicheza Malindi ya Zanzibar, alikwenda Canada kwa mkopo (loan) kwa timu ya Vancouver Whitecaps, wakati huo ikijiandaa kujiunga na MLS). Hakupata mechi rasmi, na alirudi Tanzania baada ya muda mfupi kwa sababu hakufurahishwa na hali ya huko.
Nadir alibaatizwa Jina lake la utani Canavaro, kutokana na mtindo wake wa kucheza kama beki hodari na mkali wa ulinzi, sawa na Fabio Cannavaro (mwitaliano aliyeshinda Ballon d'Or mwaka 2006).
Nadir alicheza Timu ya Taifa (Taifa Stars) hadi alipoamua kustaafu kimataifa Machi 2016.
Kwa Yanga SC, Nadir Ni moja wa wachezaji mashuhuri zaidi wa klabu hiyo, alikuwa Ni mwamba wa ulinzi, na alistaafu rasmi kucheza soka baada ya kuagwa katika mechi maalum (farewell match).
Nadir Alikuwa maarufu kwa uwezo wake wa tackling, uongozi, na kujitolea.
Kuna Mechi Nadir alibadirishana jezi na Samuel Eto'o baada ya mechi, na kulikuwa na mjadala kidogo kuhusu Jezi hiyo na TFF.
Wengi humtaja Nadir kama mmoja wa mabeki bora zaidi, katika historia ya Ligi Kuu Tanzania (hasa 2000-2020), akilinganishwa na wengine kama Victor Costa, Kelvin Yondani, au Shomari Kapombe.
Hata baada ya kustaafu, jina lake linatajwa sana katika mijadala ya Nani beki bora Nchini Tanzania.
Kwa kifupi: Nadir Ni Legend na Icon ya soka la Tanzania.
