Emam Ashour Ana ugomvi mkubwa na kocha mkuu wa Al Ahly,hii ilitokea kati kati ya juma kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Wadi Degla,baada ya mchezaji huyo kumtukana kocha wakati alipofanyiwa mabadiliko dakika 69 ya mchezo.
Kocha Jess Thorup alikasirishwa na tabia ya nyota huyo na kumchana kwamba hatokuwa sehemu ya kikosi kitakacho kuja Tanzania kuivaa Yanga.
Baada ya hapo kulitokea msuguano mkubwa kati ya kocha Jess Thorup na uongozi wa Al Ahly Baada uongozi kuonyesha wazi unamkingia kifua na kumtaka mchezaji huyo ajumuishwe kwenye Safari ya kuja Tanzania.
Jana uongozi ulijumuisha jina la Emam Ashour kwenye list ya Wachezaji watakao kuja Tanzania Ila mpaka safari inaanza Emam Ashour,hajaonekana hivyo kijana amekataa amri ya viongozi na kubaki nyumbani,ndio maana amelimwa adhabu.
Pamoja na uwezo wake uwanjani Ila Emam Ashour ni mtukutu mno
