Kocha mkuu wa Yanga SC Pedro Goncalves amesema kukosekana kwa mchezaji Emam Ashour katika cha Al Ahly akimpi matumaini ya kushinda dhidi yao, isipokuwa wanajipanga Ili wafanye vizuri siku ya mchezo, kesho.
"Ili ufanikiwe katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ukicheza dhidi ya timu kama Al Alhy ni lazima uwe tayari kwa kila aina ya nyakati ndani ya uwanja.
Kutokuwepo kwa Ashour hilo ni tatizo lao Al Ahly sisi jukumu letu ni kujiandaa vyema.” -
"Kabla ya yote tulipopangwa kwenye kundi hili kila timu ilifahamu ipo kwenye kundi gumu, sisi kama Young Africans kazi yetu ni kupambana na kila timu ili kujiweka kwenye sehemu nzuri tunapaswa kuwa bora, makini na tayari kucheza mpira mzuri ili kuwa sehemu nzuri, kuhusu mechi ya kwanza ni kweli tulicheza vizuri lakini tulifanya makosa machache ambayo kwa ubora wa wapinzani wetu walituadhibu.
Hapo kesho tunapaswa kuonesha ukuaji na ubora wetu pia ili kushinda
