WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMC FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Pongezi kwq mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliani Mkongo Fabrice Ngoy wa Ngoy dakika ya 72 kwa penalti.
Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 10 na kuruka juu kutoka nafasi ya saba hadi ya tatu, wakati KMC inayobaki na pointi zake tano za mechi 12 sasa inaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.
