Timu ya Azam FC usiku huu imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya TRA United ya mkoani Tabora mchezo wa Ligi Kuu bara uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na Jean Ngita raia wa DR Congo dakika ya 39 na Iddi Nado dakika ya 90, kwa matokeo hayo Azam FC imefikisha pointi 16 ikicheza mechi 8.
