Mayanga atupiwa virago vyake Mtibwa Sugar
Imefahamika na sasa ni rasmi klabu ya Mtibwa Sugar FC ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro, imemfuta kazi kocha wake mkuu Salum Shaban Mayanga kutokana na mwenendo wa matokeo mabovu ya timu hiyo katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara.
Baada ya kuachana na kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mtibwa Sugar kwa sasa itakuwa chini ya kaimu kocha mkuu, Awadhi Juma 'Maniche' ambaye Ataoiongoza timu hiyo Katika mechi zilizosalia mpaka mwishoni mwa msimu huu.