MASHABIKI SIMBA WAMIMINIKA LEO KUIPOKEA TIMU YAO IKITOKA MOROCCO
Na Shafih Matuwa
Mashabiki wa waliokuwa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, Simba SC, lwameweka historia ya kwenda kuipokea timu yao iliyotokea nchini Morocco.
Simba juzi iliondolewa katika michuano hiyo baada ya kufungwa mabao 4-3 na timu ya Wydad Casablanca yaliyopatikana kwa changamoto ya penalti hasa baada ya kutoka sare 1-1 ndani ya dakika 180.
Mashabiki wa Simba waliamua kujitokeza kwa wingi uwanja wa ndege wa JK Nyerere jijini Dar es Salaam kuwapokea wachezaji wao na kuwapa moyo.
Wachezaji wa Simba wanastahili mapokezi hayo kwani walipambana vya kutosha na kuwabana wenyeji wao kiasi kwamba waliambulia ushindi kiduchu wa 1-0 na kupelekea changamoto ya penalti tano kwa tano.
Simba nayo ilipata ushindi kiduchu jijini Dar es Salaam wa bao 1-0