Simba yaanza safari ya kurejea nyumbani
Baada ya jana usiku kuondoshwa kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, kikosi cha wachezaji wa Simba SC kimeanza safari ya kurejea nchini Tanzania.
Simba jana ilitupwa nje ya michuano hiyo ilipofungwa na Wydad Casablanca kwa changamoto ya penalti 4-3 hasa baada ya kutoka sare ya mabao 1-1 ndani ya muda wa dakika 180.
Katika mchezo wa jana Simba ilifungwa bao 1-0 goli lililofungwa na mshambuliaji Bouly Sambou raia wa Senegal, mchezo uliofanyika uwanja wa Mohamed wa 5 mjini Casablaca.
Lakini Simba ilikuwa ya kwanza jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Mkapa kuifunga Wydad pia 1-0 likifungwa na mshambuliaji wake Jean Baleke raia wa DR Congo, Simba sasa inaenda kushiriki Ligi Kuu bara, kombe la FA na michuano ya Super League pekee baada ya kuondoshwa Ligi ya mabingwa.