Baloteli ajutia makosa yake hadi Messi na Ronaldo kushinda Ballon d'Or nyingi
Ni kosa langu Messi na Ronaldo kuwa na Ballon d'Or nyingi- Balotelli
Mtukutu Super Mario Balotelli amedai kuwa ni makosa yake Messi na Ronaldo kuwa na wingi wa Ballon d'Or.
Kupitia Muschio Selvaggio, Balotelli amesema wakala wake wa zamani, Mino Raiola alimwambia anauwezo mkubwa uwanjani kiasi kwamba kuwazidi Messi na Ronaldo na hata kuvunja utawala wao wa miaka 12 wa tuzo za Ballon d'Or.
Mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 32 anaamini kama sio utukutu na ukorofi wake basi angekuwa na mafanikio makubwa na kuleta ushindani mkali mbele ya Messi na Ronaldo.
"Raiola mara zote amekuwa akiniambia jambo moja tu, kama Messi na Cristiano Ronaldo wanakuwa na tuzo nyingi za Ballon d'Or ni makosa yako,” amesema Balotelli ambaye kwa sasa anakipiga FC Sion.
Balottelli ameongeza kuwa "Wakala Raiola alikuwa sahihi, nilikuwa nacheza asilimia 20 tu ya uwezo wangu.”
Mwishoni mwa mwaka 2000 Mshambuliaji huyo alikuwa wamoto kweli kweli akiitumikia Inter Milan na kuhesabika kijana mwenye kipaji zaidi barani Ulaya.
Dili lake la kusajiliwa na Manchester City lilikuwa euro milioni 29.5 lakini pia akitwaa tizo ya Golden Boy kwa kuwa mchezaji bora mwenye umri mdogo wa miaka 21 na mwaka huo akiwa mchezaji muhimu ndani ya timu ya taifa ya Italia.