Fountain Gate walia na Kitayonce, wadai inatoa rushwabkupanda Ligi Kuu
Baada ya mchezo kati ya Fountain Gate FC dhidi ya Kitayosce FC kutamatika, mmoja wa kiongozi wa klabu ya Fountain Gate alizungumza na waandishi wa habari huku akiushutumu uongozi wa klabu ya Kitayosce kuhusika na vitendo vya rushwa
Katika hatua nyingine aliwaambia waandishi wa habari kwamba kabla ya mchezo huo mmoja wa kiongozi wa Kitayosce alituma kiasi cha fedha Kwa wachezaji wa Fountain Gate FC ili kurahisisha matokeo ya mchezo huo.
Alisema pia kama viongozi wameripoti tukio hilo polisi huku tayari mchakato wa kuripoti tukio hilo Shirikisho la Soka nchini TFF ili kuona haki inatendeka