Ndanda yajitoa Ligi daraja la kwanza bara
NDANDA WAKUBALI YAISHE
Klabu ya Ndanda ya Mtwara imetangaza kujitoa katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship), huku sababu ikielezwa ni ukata kiasi Cha kushindwa kumudu gharama za kujiendesha.
Timu hiyo ilipaswa kusafiri kuelekea mkoani Mwanza kwa ajili mchezo dhidi ya COPCO Veteran lakini walikosa fedha za kugharamia safari hiyo.
Baada ya hali hiyo Uongozi umetangaza kujitoa rasmi kwenye Ligi hiyo huku ukisisitiza walijaribu kuwashirikisha wadau mbalimbali ili wapate msaada lakini ilishindikana.
Ndanda inakuwa ni timu ya pili msimu huu kujitoa katika Ligi Daraja la Kwanza (Championship) baada timu ya Gwambina kufanya hivyo katikati ya Msimu wa Ligi.