AZAM FC WAJINASIBU KUFANYA VIZURI MSIMU UJAO AFRIKA
Uongozi wa klabu ya Azam FC ‘Wanalamba lamba’ umesema, watahakikisha msimu ujao wa mwaka 2023-24 wanafanikiwa kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa kwa kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.
Mkurugenzi Mtendaji wa klabu ya Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ameiambia EATV kuwa, mpaka sasa wameshajihakikishia nafasi ya ushiriki wa kombe la shirikisho barani Afrika hivyo wanaendelea kuweka mipango ya kuboresha benchi la Ufundi na wachezaji.