YANGA KUTINGA NUSU FAINALI LEO?
Na Salum Fikiri Jr
WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika michuano ya kimataifa Dar Young Africans, maarufu Yanga SC usiku wa saa moja watashuka dimbani kuikaribisha timu ya Rivers United ya Nigeria kucheza mechi ya marudiano ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika.
Katika mchezo huo utakaofanyika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, Yanga inahitaji sare yoyote ama kufungwa goli moja ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali hasa baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Nigeria.
Hata hivyo mechi hiyo itakuwa ngumu kwani Rivers hawatakubali kutolewa kwenye hatua hiyo ya robo fainali na watapambana ili kulipiza kisasi na kushinda zaidi ya magoli mawili ili waweze kuingia nusu fainali.
Lakini Yanga nao wanaonekana kukamia vikali na kupata ushindi ili wawape furaha mashabiki wake, mshambuliaji hatari wa timu hiyo Mkongoman Fiston Mayele ambaye katika mchezo wa kwanza uliofanyika Nigeria aliweza kufunga magoli yote mawili, hivyo leo atataka kuendeleza makali yake.
Pia Mayele alisikika hivi karibuni akiwaomba wachezaji wenzake ya Yanga wampe ushirikiano ili aweze kushinda tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo, mpaka sasa Mayele ana mabao matano na anafungana na mshambuliaji wa Malumo Galaxy Ranga Chivavulo