WYDAD CASABLANCA YAITOA SIMBA NA KUTINGA NUSU FAINALI
Na Prince Hoza
Mabingwa watetezi wa Ligi ya mabingwa barani Afrika, Wydad Casablanca ya Morocco usiku huu imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuifunga Simba SC ya Tanzania mabao 4-3 kwa mikwaju ya penalti kutokana na sare ya 1-1 ndani ya dakika 180.
Katika mchezo wa leo Wydad ilipata ushindi wa bao 1-0 na kufanya timu hizo kufungana 1-1 kwani Simba nayo ilipata ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wake wa nyumbani wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa leo umefanyika katika uwanja wa Mohamed wa 5 uliopo mjini Casablanca ambapo Bouly Sambou alifunga goli pekee la ushindi lililopelekea timu hizo kupigiana penalti.
Shomari Kapombe na Clatous Chama ndio wachezaji wa Simba waliopoteza mikwaju ya penalti, Simba sasa wameshindwa kufika nusu fainali na kama kawaida yao kutolewa kwenye hatua ya robo fainali