Machapisho

Ally Kiba kupamba Simba Day

Picha
Klabu ya Simba SC imemtangaza rasmi mwanamuziki Alikiba kuwa msanii mkuu atakayetumbuiza katika tamasha la Simba Day mwaka huu. ​Hatua hii inalenga kuongeza thamani ya burudani na hamasa kwa mashabiki na wadau wa soka kuelekea utambulisho wa kikosi cha msimu ujao.

Yanga mwendo wa 7

Picha
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC, Young Africans (Yanga SC), wameendelea kuonyesha utulivu na uwezo mkubwa wa ushambuliaji baada ya kuibuka na ushindi mnono wa magoli 7-0 dhidi ya klabu ya Kigamboni United (B-19) inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship). ​Katika mchezo huo wa kujiandaa na msimu mpya, safu ya ushambuliaji na viungo wa Yanga ilionyesha utofauti mkubwa kupitia mchanganyiko wa wachezaji wapya na wa zamani waliopachika mabao hayo: ​⚽ Wafungaji wa Magoli ya Yanga SC: ​Erick Mwijage ⚽ (Assist: Mihambo) ​Cheikh Ibrahima Touré ⚽ (Penati) ​Cheikh Ibrahima Touré ⚽ (Assist: Mohamed Hussein 'Zimbwe') ​Kazimoto ⚽ ​Kazimoto ⚽ (Assist: Hussein Zakuani) ​Hussein Zakuani ⚽ (Assist: Cheikh Touré) ​Maxi Nzengeli ⚽ (Assist: Chadrack Boka) ​Ushindi huu wa magoli saba unakuwa wa pili mtawalia katika mechi za majaribio, ukionyesha kuwa kikosi hicho kinaendelea kuimarika kwa kasi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii pamoja na msimu mpya wa mashindano.

Karia aahidi kuwadhibiti wanaotumia gesi vyumba vya kubadilishia

Picha
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema TFF inanunua vifaa maalum vitakavyotumika kuthibitisha uwepo wa gesi katika maeneo ya vyumba vya kubadilishia nguo. Karia amesema matukio hayo yanaripotiwa kufanyika, lakini TFF inataka kupata ushahidi wa kitaalamu kabla ya kuchukua hatua dhidi ya timu husika. Wallace Karia: "Tunanunua vifaa maalum vya kuthibitisha uwepo wa gesi na ni kweli hayo mambo yanafanyika. Lakini ikiwa tutajiridhisha timu imevalia nje ya vyumba na tukabaini hakuna sumu au harufu hizo, itapokwa pointi 5. "Kauli hiyo imekuja wakati TFF ikiweka msisitizo wa kuhakikisha matukio yanayodaiwa kutokea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo yanathibitishwa kwa ushahidi kabla ya hatua za kinidhamu kuchukuliwa.

Haroub awashukuru viongozi Simba

Picha
“Viongozi wamenituma kuja kueleza machache kubwa zaidi ni kuwashukuru wenzetu wa Ngorongoro kwa ushirikiano huu, lakini pia kuwashukuru wadhamini wetu wanaowezesha klabu hii kuwa kubwa. Tuunge mkono timu yetu, tumesajili vizuri, tuna malengo ya kufika mbali kwenye michuano ya Afrika na michuano ya ndani. Huu ni mwaka wetu Wanasimba na sherehe hizi zinakwenda sambamba na sherehe za miaka 90 tangu kuanzishwa kwa Klabu ya Simba.”- Mjumbe wa Bodi, Selemani Haroub kwenye uzinduzi wa Simba Week 2026.

Simba yazindua jezi mpya

Picha
Klabu ya Simba SC hii leo imetambulisha jezi zake mpya kwa ajili ya msimu ujao, Simba imetambulisha jezi hizo ambazo watazitumia kwenye mashindano ya ligi za ndani na mechi za kirafiki.

Simba nje Kagame Cup ikishinda 2-1

Picha
Timu ya Simba SC imefanikiwa kuambulia ushindi kwenye kombe la Kagame Cup baada ya kuifunga Singida Black Stars mabao 2-1 uwanja wa Amahoro jijini Kigali Rwanda. Mabao ya Simba yamefungwa na Ibrahim Doumbia dakika ya 27 na Elie Mpanzu dakika ya 66 wakati goli la Singida lilifungwa na Mathew Tegisia Momanyi dakika ya 55 na timu zote zimeaga mashindano hayo kufuatia pointi zao hazikuivuka Jamus ambayo imeingia nusu fainali kwa kufikisha pointi 7

Kocha wa Bafana Bafana ajiuzuru

Picha
Kocha Hugo Broos amejiuzulu nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) baada ya kuhudumu kwa miaka mitano!. Hugo amejiuzulu baada ya kumalizika kwa michuano ya FIFA World Cup 2026 na Afrika Kusini wapo wanatafuta mbadala wake mapema sana.

Fred Ngoma ni mwananchi

Picha
Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mkabaji namba 6, Fred Duval Ngoma, raia wa Jamhuri ya Congo Brazzaville, akitokea klabu ya Olympique de Safi inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco Botola Pro. Ngoma, mwenye umri wa miaka 28, anatajwa kuwa miongoni mwa viungo wenye uwezo mkubwa wa kucheza mbele ya safu ya ulinzi kutokana na uwezo wake wa kukaba, Mbali na nafasi yake ya kiungo mkabaji, pia ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa kati pale inapohitajika. Katika msimu wa 2025,26 akiwa na Olympique de Safi, Ngoma alikuwa mchezaji muhimu wa kikosi hicho, akicheza mechi nyingi za ligi na kuonyesha kiwango cha juu cha uthabiti katikati ya uwanja. Kabla ya kutua Morocco, aliwahi kuzichezea klabu mbalimbali barani Afrika na pia amewahi kuitwa katika timu ya taifa ya Congo Brazzaville. Usajili wa Fred Ngoma unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa Yanga kuimarisha safu ya kiungo kuelekea msimu mpya wa mashindano ya ndani pamoja na michuano ya kimataifa.Ujio wake unatarajiwa kuongeza ushindani mkub...

Yanga na Simba kupigwa New Amaan Stadium

Picha
Mechi ya kuashiria kuanza Ligi Kuu ya NBC Primier League 2026/2027 Ngao ya Jamii inatarajia kuchezwa kwenye uwanja wa New Amaan Stadium mjini Zanzibar. Mechi hiyo iliyopangwa Agosti 12 mwaka huu inayokutanishwa watani wa jadi Yanga na Simba, itachezwa uwanja huo usiku saa 2' 30, Bodi ya Ligi wameelekeza mechi kufanyika Amaan Stadium badala ya uwanja wa Uhuru.

Nyota Yanga ateuliwa Rais wa klabu DR Congo

Picha
Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, David Molinga 'Falcao' raia wa DR Congo, ameingia kwenye historia mpya katika maisha yake ya soka baada ya kuchaguliwa rasmi kuwa Rais wa Klabu ya AC Bandal kwa mkataba wa miaka mitano.  AC Bandal ni klabu yenye makao yake katika wilaya ya Bandalungwa mjini Kinshasa inayoshiriki Ligi ya EUFKIN-Malebo, na pia ni timu ambayo Molinga mwenyewe aliwahi kuitumikia zamani kama mchezaji. Kupitia ujumbe wake wa shukrani, Molinga amemshukuru Mwenyezi Mungu na kueleza fahari yake kubwa kupewa dhamana ya kuiongoza klabu hiyo iliyowahi kutwaa ubingwa wa Super Coupe ya Kinshasa mwaka 2014.  Amewaahidi wanachama, viongozi na mashabiki kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uwazi ili kuijenga AC Bandal kuwa klabu imara na yenye mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja. Uamuzi huu unamfanya 'Falcao' kujiunga na orodha ya wachezaji wa zamani barani Afrika waliofanikiwa kubadilisha viatu vya soka na kuvaa suti za uongozi katika ngazi ya juu y...

Barker aujia juu uongozi Simba, aponda usajili

Picha
Taarifa zinazoendelea kuzungumzwa ndani ya Simba SC zinaeleza kuwa kocha mkuu Steve Barker hakuwa ameridhishwa na baadhi ya usajili uliofanywa na klabu hiyo kuelekea msimu mpya. Inaelezwa kuwa Barker aliwasilisha mapendekezo yake ya wachezaji aliotaka kuimarisha kikosi, lakini si mapendekezo yote yaliyotekelezwa na uongozi. Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya wachezaji waliosajiliwa hawakuwa sehemu ya chaguo la kwanza la kocha huyo. Majina yanayotajwa ni pamoja na mshambuliaji Doumbia, Chilambo na Jabaar, huku ikielezwa kuwa usajili wao ulifanyika kutokana na maamuzi ya uongozi badala ya mapendekezo ya benchi la ufundi. Aidha, Barker anaripotiwa kushangazwa na kushindwa kwa klabu kukamilisha baadhi ya mahitaji aliyoyaona kuwa ya msingi. Miongoni mwa hoja zinazotajwa ni kushindwa kufanikisha makubaliano yaliyohitaji malipo ya $50,000 kwa Wydad ili kuendelea na mchakato wa kumpata Selemani Gomez, jambo ambalo linaelezwa kuwa lilikuwa sehemu ya vipaumbele vyake katika kuimarisha kikosi...

Zougrana atambulishwa Yanga apewa jezi namba 6

Picha
Klabu ya Yanga SC imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya wa mashindano kwa kukamilisha usajili wa kiungo mahiri Mohamed Tchapi Zougrana, ambaye sasa amepatiwa jezi namba 6. Nyota huyu mwenye umri wa miaka 25 na raia wa Burkina Faso amejiunga na Wananchi akitokea MC Alger ya Algeria, baada ya awali pia kuitumikia ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Zougrana anatambulika kwa uwezo wake wa kucheza nafasi ya kiungo wa kati kwa ustadi mkubwa. Ni mchezaji mwenye sifa ya kukaba kwa ufanisi, kumiliki mpira na kuanzisha mashambulizi kwa pasi sahihi. Uwezo huu unamfanya kuwa nyota wa kipekee ambaye anaweza kuimarisha safu ya kiungo ya Yanga SC na kuongeza ubunifu wa kikosi katika mechi ngumu. Jezi namba 6, ambayo mara nyingi huhusishwa na wachezaji wa kiungo wa kati wenye jukumu la kudhibiti mchezo, ni ishara ya imani kubwa ya klabu kwa uwezo wake.

Allan Okello amtaja aliyempeleka Yanga

Picha
Kiungo wa kimataifa wa Uganda, Allan Okello, amefunguka kuhusu mchango wa Dr Lawrence Mulindwa katika safari yake ya kujiunga na Yanga SC, akimtaja kama mtu mwenye nafasi kubwa katika maisha yake. Allan Okello amesema Dr Lawrence Mulindwa ni zaidi ya mshauri kwake, akieleza kuwa anamchukulia kama baba na mlezi aliyekuwa akimuongoza katika hatua mbalimbali za maisha yake ya soka.Okello amesema Mulindwa alimshauri asisite kutumia nafasi ya kuhamia Yanga SC na kumtaka aende Tanzania kuonyesha uwezo wake. Allan Okello: "Dr Lawrence Mulindwa ni kama baba kwangu. Ni mlezi wangu. Aliniambia nitumie fursa hii ya uhamisho kwenda Yanga na nikaitawale Tanzania."Ujumbe huo unaonyesha namna Mulindwa alivyompa Okello moyo na ushauri katika hatua yake ya kuanza sura mpya ya soka nchini Tanzania. # Allan Okello

Ahoua kimeeleweka Jordan

Picha
Mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2024/25, Jean Ahoua ametangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Al-Faisaly SC ya Nchini Jordan akitokea klabu ya CR Belouizdad ya Algeria. Nyota huyo wa zamani wa Simba SC, raia wa Ivory Coast, amejiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru baada ya kusitisha mkataba wake na CR Belouizdad kwa makubaliano ya pande zote mbili, akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia miamba hiyo ya Jordanian Pro League. Ahoua 24 alijiunga na Simba SC mnamo Julai 2024 na kuitumikia klabu hiyo Kwa msimu mmoja na nusu ambapo aliisaidia miamba hiyo ya Dar es Salaam kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2025 huku akiwa kinara wa magoli kwenye Ligi kuu bara akifikisha jumla ya magoli 16 kwenye ligi hiyo msimu wa 2024/25. Mnamo Januari 2026 Simba SC alimuuza nyota huyo wa zamani wa Stella Club d'Adjamé ya Nchini kwao Ivory Coast kwenda CR Belouizdad na kuhudumu kwa miamba hiyo ya Algeria kwa nusu msimu.

SAJILI ZA MAJINA MAKUBWA...

Picha
Na Prince Hoza Matua PETER Shalulile ni jina kubwa lililotambulishwa mwanzoni mwa wiki hii ikiwa ni usajili wa klabu ya Yanga SC, huo ni usajili wa nne kati ya maproo waliowasajili msimu huu na kwa mujibu wa viongozi bado wachezaji wakubwa kuwatsngaza. Shalulile ni mchezaji mkubwa barani Afrika, alikuwa anaichezea timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji walioipa jina timu hiyo kutokana na mafanikio yake. Rekodi nzuri ya kufunga hasa kwenye ligi za ndani na kimataifa imemuweka kwenye wakati mzuri kama mchezaji, Shalulile ni mshambuliaji wa kati alikuwa na wastani wa kufunga magoli zaidi ya 20 hivyo aliibuka kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo. Shalulile amewahi kubeba CAF Champions League, pia ameshinda mara kadhaa ubingwa wa nchi hiyo na makombe mengine  ya ndani, ni mmoja kati ya wachezaji wenye sifa kemkem nchini humo. Sidhani kama kuna timu nje ya Afrika Kusini ambayo haina shauku na mchezaji huyo mwenye uraia wa Namibia, Yanga SC...

SAJILI ZA MAJINA MAKUBWA...

Picha
Na Prince Hoza Matua PETER Shalulile ni jina kubwa lililotambulishwa mwanzoni mwa wiki hii ikiwa ni usajili wa klabu ya Yanga SC, huo ni usajili wa nne kati ya maproo waliowasajili msimu huu na kwa mujibu wa viongozi bado wachezaji wakubwa kuwatsngaza. Shalulile ni mchezaji mkubwa barani Afrika, alikuwa anaichezea timu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji walioipa jina timu hiyo kutokana na mafanikio yake. Rekodi nzuri ya kufunga hasa kwenye ligi za ndani na kimataifa imemuweka kwenye wakati mzuri kama mchezaji, Shalulile ni mshambuliaji wa kati alikuwa na wastani wa kufunga magoli zaidi ya 20 hivyo aliibuka kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo. Shalulile amewahi kubeba CAF Champions League, pia ameshinda mara kadhaa ubingwa wa nchi hiyo na makombe mengine  ya ndani, ni mmoja kati ya wachezaji wenye sifa kemkem nchini humo. Sidhani kama kuna timu nje ya Afrika Kusini ambayo haina shauku na mchezaji huyo mwenye uraia wa Namibia, Yanga SC...

Simba yatupwa nje Kagame Cup

Picha
Simba SC imehitimisha rasmi safari yake katika michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026 baada ya kushindwa kufuzu hatua ya nusu fainali kufuatia matokeo ya michezo ya hatua ya makundi. Baada ya kukusanya pointi mbili pekee katika michezo yake miwili ya kwanza, Simba ilijikuta katika nafasi ngumu ya kusonga mbele. Hata kama itaibuka na ushindi katika mchezo wake wa mwisho dhidi ya Singida Black Stars na kufikisha pointi tano, idadi hiyo haitatosha kuiwezesha kuwa miongoni mwa timu bora zilizomaliza katika nafasi ya pili zitakazofuzu hatua inayofuata. Hali hiyo imechangiwa na matokeo ya makundi mengine, ambapo Al Hilal na Rayon Sports tayari zimekusanya pointi sita kila moja, na hivyo kuondoa uwezekano wa Simba kuingia katika orodha ya timu zitakazofuzu nusu fainali. Kutokana na matokeo hayo, Simba SC inaaga rasmi michuano ya CECAFA Kagame Cup 2026 na sasa itaelekeza nguvu zake katika kujiandaa na msimu mpya wa mashindano ya ndani na kimataifa.

Wydad yamrejesha kundini Seleman Mwalimu "Gomez"

Picha
Selemani Mwalimu yupo jijini Dar Es Salaam akishughulikia safari yake ya kuelekea Morocco kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya. Kocha mpya wa Wydad, Paulo Sergio anataka kuwaona wachezaji wote kambini kabla ya kufanya maamuzi.

Yanga yazima tetesi za Feitoto kutua Yanga'

Picha
Baada ya kuzagaa kwa tetesi zinazomhusisha kiungo wa Azam FC, Feisal Salum, na kujiunga na Yanga, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ally Kamwe, amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea kati ya pande hizo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kamwe amesema Yanga tayari imekamilisha usajili wa wachezaji wa ndani, hivyo Feisal si sehemu ya mipango ya klabu hiyo. "Feisal Salum ni mchezaji mzuri sana, lakini Yanga SC tumeshafunga usajili wetu wa ndani. Hakuna mazungumzo yoyote kati ya Yanga na Fei/Azam," ameandika Kamwe. Aidha, ameeleza kuwa nafasi mbili za usajili zilizobaki klabuni hapo ni kwa ajili ya wachezaji wa kimataifa pekee.

Al Hilal yaitoa mashindanoni KVZ

Picha
Al Hilal imepata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya KVZ katika mchezo wa mzunguko wa pili wa kundi C la CECAFA Kagame cup 2026. Ushindi huu unawafanya Al Hilal wapande kwenye kilele cha msimamo wa kundi C wakiwa na points zao 6. Mchezo wa kundi C unaofuata hivi punde ni kati ya Rayon Sports dhidi ya Tusker FC.