Karia aahidi kuwadhibiti wanaotumia gesi vyumba vya kubadilishia
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amesema TFF inanunua vifaa maalum vitakavyotumika kuthibitisha uwepo wa gesi katika maeneo ya vyumba vya kubadilishia nguo.
Karia amesema matukio hayo yanaripotiwa kufanyika, lakini TFF inataka kupata ushahidi wa kitaalamu kabla ya kuchukua hatua dhidi ya timu husika.
Wallace Karia: "Tunanunua vifaa maalum vya kuthibitisha uwepo wa gesi na ni kweli hayo mambo yanafanyika. Lakini ikiwa tutajiridhisha timu imevalia nje ya vyumba na tukabaini hakuna sumu au harufu hizo, itapokwa pointi 5.
"Kauli hiyo imekuja wakati TFF ikiweka msisitizo wa kuhakikisha matukio yanayodaiwa kutokea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo yanathibitishwa kwa ushahidi kabla ya hatua za kinidhamu kuchukuliwa.
