MKOLA MAN AGEUKIA MALAVIDAVI

STAA wa ngoma ya ‘Mr Mapesa iliyosumbua sana katika vituo vya redio Christopher Mhenga ‘Mkola Man’ majuzi kati aliachia ngoma nyingine ya mapenzi ‘malovedav time’ katika studio za Hekman Record zilizopo jijini Dar es salaam chini ya prodyuza Galaton Money Devil.

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili, Mkola Man alisema ameamua kutengeneza wimbo wa mapenzi kutokana na muda uliopo, ‘nimeona nifanye wimbo wa mapenzi kwa sababu huu ndio wakati wake, hakuna asiyejua utamu wa mapenzi, kila siku naimba nyimbo za kigumu sasa nimekuja kumridhisha wangu mpenzi’, alisema Mkola Man.

Wimbo huo ameamua kumshirikisha mshirika wake wa karibu Yusa G, Amour Jay na Fabby ‘Bamaboy’, Mkola Man anamshukuru sana meneja wake Dk Sakaingo ‘Big Boss’ ambaye amemwezesha kurekodi wimbo huo na kugharamia mambo mengine.


Mkola Man ambaye maskani yake jijini Tanga lakini ameamua kuja kurekodi ngoma yake mpya jijini Dar es Salaam kutokana na kwenda na wakati uliopo, ‘Dar es Salaam ndio kila kitu mambo yote yanafanyika hapa hivyo ni bora nije kufanya ngoma hapa lakini bado naishi Tanga jiji la wajanja’, alisema huku akicheka.

Mkola Man ameongeza bado ataendelea kumuheshimu prodyuza wake Mosi a k a Division One aliyemtengenezea wimbo wake wa Mr Mapesa ambao ndio uliomuweka kwenye ramani ya muziki hapa nchini, Mkola Man amewaomba mashabiki wake kumpokea tena kama walivyompokea kwenye wimbo wake wa Mr Mapesa na nyinginezo.

Msanii huyo kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiandikwa sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kuhusishwa na freemason ingawa yeye mwenyewe amedai ni uzushi tu anaopakaziwa na watu ili kumuharibia jina lake wakati yeye ni mtoto wa kilokole aliyelelewa katika mazingira ya kiroho

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA