LIVERPOOL YAANZA MAZUNGUMZO MAPYA NA STERLING

Raheem Sterling 

Afisa Mkuu Mtendaji wa Liverpool, Ian Ayre, amefanya mazungumzo na waakilishi wa Raheem Sterling kuhusu mkataba mpya, meneja Brendan Rodgers amefichua.

Rodgers alishikamana kuwa klabu hicho cha ligi ya Premier ya Uingereza kina ‘utulivu’ kuhusu mshambuliaji huyo chipukizi nyota licha ya taarifa anaweza kuondoka.
Mchezaji huyo wa wingi wa Uingereza amehusishwa na miamba wa Uhispania, Real Madrid kufuatia ripoti kuwa hana makini ya kuongeza muda katika kandarasi yake na Liverpool inayodumu hadi 2017.


“Ian Ayre ameongea na maagenti wake na hana wasiwasi wowote, Klabu hiki kinajadiliana na wakala wake na mambo ni tulivu. Kijana huyo ana raha nyingi hapa na hana mawazo tofauti kuhusu kuchezea Liverpool,” Rodgers alisema.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA