HISPANIA YAIBUKA KIDEDEA MATAIFA ULAYA

Harakati za kutafuta tiketi ya kufuzu kuelekea nchini Ufaransa mwaka 2016 kwenye michuano ya soka ya mataifa bara la Ulaya ziliendelea tena usiku wa kuamkia leo wakati timu kadhaa ziliposhuka dimbani.


Mabingwa watetezi Hispania walikuwa wageni dhidi ya Luxembourg , hadi mwisho wa mchezo huo wageni Hispania wakafanikiwa kuibuka washindi baada ya kuwaadhibu wenyeji wao kwa jumla ya mabao 4-o. Russia ilishindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubali kugawana point na wageni wao Moldova kwa kutoka sare ya bao 1-1.

Kwingineko England iliibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Estonia.Nayo Swedeni nako kulikuwa na hekaheka zilizowakutanisha wenyeji Sweden dhidi ya Liechtenstein.

Hadi mwisho wa mchezo huo wenyeji wakafanikiwa kuwagaragaza wapinzani wao kwa jumla ya mabao 2 kwa mshangao.Austria ikaisambaratisha Montenegro kwa jumla ya goli 1 kwa bila, wakati Slovenia walipowavunjia heshima wenyeji wao Lithuania kwa kuwasasambua bila huruma kwa mabao 2-0 huku Belarus ikitafuta majibu ya kuwapa mashabiki wake baada ya kudondokea pua kwakufungwa mabao 3-1 dhidi ya Slovakia.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA