MAKALA: SIMBA NA YANGA NI MABOMU YANAYOSUBIRI ZAMU YA KULIPUKA
Na Prince Hoza
NINGEANZA kwa pongezi kwa timu ya taifa, Taifa Stars ambapo
mwshoni mwa wiki ilifanikiwa kuilaza timu ngumu ya taifa ya Benin katika mchezo
wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa na shirikisho la soka duniani Fifa,
mchezo huo ulifanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kufanyika mchezo huo kulitanguliwa na mchezo wa
kirafiki kati ya waumini wa dini mbili za Kiislamu na Kikristo, katika mchezo
huo waumini hao walijigawanya katika timu mbili na moja iliitwa Amani na
nyingine iliitwa Mshikamano, Aman ilishinda 1-0 goli likifungwa na Sheikh mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam.
Vile vile klabu ya Simba bado iko nchini Afrika Kusini
ikijiandaa na mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya hasimu wake mkuu Yanga, Simba
imeamua kuweka kambi nchini humo na kucheza mechi mbili za kajaribio.
Timu hizo zote zinaingia uwanjani zikiwa tayari zimeshacheza
mechi tatu kila mmoja, Simba ilianza ligi kwa kucheza na Coastal Union ya Tanga
katika uwanja wa Taifa ambapo matokeo yalikuwa sare ya kufungana 2-2, aidha
ilishuka tena katika uwanja huo huo wa Taifa na kucheza na Polisi Moro ambapo
matokeo yaliendelea kuwa sare ya 1-1.
Matokeo hayo yaliwaudhi mashabiki wake hasa kutokana na
usajili wa msimu huu Simba imeonekana kuimarika, Simba iliwasajili nyota
Emmanuel Okwi, Pierre Kwizera, Manyika Peter, Hussein Sharrif ‘Casilass’, Paul
Kiongera, Ibrahim Hajibu, Joram Mgeveke na wengineo.
Pia iliimarisha benchi la ufundi kwa kumrejesha aliyekuwa
kocha wake mwewnye mafanikio na timu hiyo Mzambia Patrick Phiri, awali Simba
ilikuwa ikinolewa na Mcrotia Zdravko Logarusic, kuajiliwa kwa Phiri na
kusajiliwa kwa Okwi na Kiongera kumewafanya mashabiki wa Simba kutembea vifua
mbele.
Okwi anafahamika kwa kiwango chake cha juu na Kiongera
alianza kuwaonyesha mavitu mashabiki wa Simba katika mecho za kirafiki,
mchezaji huyo raia wa Kenya alionyesha uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na
kuwapa matumaini mashabiki wa timu hiyo.
Hata hivyo Simba imeanza ligi vibaya kwa kutoka sare mechi
tatu mfululizo, Simba ilikuwa kambini visiwani Zanzibar ambapo ilicheza mechi
kadhaa za kirafiki kabla haijarejea kuanza ligi, mchezo wa tatu wa Simba
ilicheza na Stand United ya Shinyanga katika uwanja wa Taifa ambapo matokeo
yalikuwa 1-1.
Kutokana na mwenendo huo mbaya was are ilioanza nao Simba
imeamua kuondoka nchini na kukimbilia Afrika Kusini huenda mambo yakabadilika,
pia tayari minong’ono ya chini kwa chini imeanza katika klabu ya Simba ambapo
kuna watu wanahusishwa na matokeo hayo, inasemekana kundi la wanachama
waliosimamishwa maarufu kama Ukawa ndio wanaotupiwa macho.
Marcio Maximo akiwa na straika anayemuamini Jaja, lakini Yanga ikifungwa na Simba ujue lawama inamndokea yeye kwa kumbeba Mbrazil mwenzake
Ingawa hakuna ushahidi wowote kama wanahu7sika moja kwa moja
lakini wanachama hao nano wamekuwa na ishara zao zinazoashiria kuna mgogoro
unafukuta ndani ya Simba, lakini kuna malalamiko mengine kuwa uongozi wa sasa
wa Simba chini ya rais Evans Aveva umewabagua wazee wa klabu hiyo wakiongonzwa
na mzee Hamisi Kilomoni.
Kuwatimua wazee hao kumepelekea baadhi ya mambo kuyumba,
hivyo kuna uwezekano mkubwa Simba ikaanza ligi na mtani wake kwa furaha ama
kupoteza au kuendelea na sare zake kama kawaida, Kwa upande wa Yanga nako ni
hivyo hivyo kama Simba ingawa kuna tofauti kidogo.
Kikosi cha Yanga kiliweka kambi yake Visiwani Pemba,
ilicheza mechi kadhaa za kirafiki kabla ya haijaingia katika mechi za ligi,
Yanga nayo imefanya usajili wake makini msimu huu kwa kuwasajili Wabrazil
Andrey Coutinho na Geilson Santana Santos Jaja, pia iliimarisha benchi lake la
ufundi baada ya kuondokewa na mwalimu wake Mholanzi Hans Van Der Pluijm na
msaidizi wake Charles Boniface Mkwassa.
Yanga iliamua kumchukua aliyekuwa kocha wa timu ya taifa,
Taifa Stars Mbrazil Marcio Maximo, pia ikamchukua msaidizi wa Maximo ambaye
naye ni Mbrazil Leonaldo Neiva, Yanga iliendelea kuimarisha benchi lake la
ufundi kwa kuwaajili wachezaji wake wa zamani Shadrack Nsajigwa na Salvatory
Edward kuwa makocha wasaidizi.
Yanga ilianza ligi vibaya kwa kupoteza dhidi ya Mtibwa Sugar
mchezo uliofanyika mjini Morogoro kwenye uwanja wa Jamhuri, pia ikafufua
matumaini yake kwa kuzilaza Prisons ya Mbeya na JKT Ruvu ya Pwani mabao 2-1 ,
Yanga imefikisha pointi sita huku mtani wake Simba akiwa na pointi 3.
Karibu vikosi vya timu zote vipo imara na kila mmoja
anatambia kikosi chake hivyo tarehe 18 ndiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa,
lakini vilabu hivi kila vinapokutana vimekuwa na kila aina ya tambo na mmoja
wapo anapopoteza mchezo huanza kunagusha lawama kwa benchi lake la ufundi au
wachezaji.
Utasikia mchezaji Fulani amehujumu, au kocha awezi kazi
ameshindwa kuendana na timu yetu, tayari timu hizo zimefukuza makocha wengi
katika kipindi cha miaka miwil, Yanga tangia 2009-2014 imeshatimua makocha
zaidi sita wakati mtani wake Simba naye ni hivyo hivyo.
Timu timua yao inatokana na mchezo wa Simba na Yanga au
kuvurunda katika mechi kadhaa na kuinyima timu ubingwa, siwezi kushangaa
kusikia Yanga imemtimua kocha wake baada ya kufungwa na Simba, au Simba
imemtimua kocha wake baada ya kufungwa na Yanga.
Sitashangaa kusikia mchezaji Fulani kasimamishwa na Yanga
kufuatia matokeo mabovu dhidi ya Simba au Simba imemtimua mchezaji wake Fulani kufuatia
matokeo mabovu dhidi ya Yanga, timu hizi ni kama bomu linalosubiri kulipuka.
Vuguvugu la chini kwa chini lililopo Simba mwisho wake
litamalizika kwa mpambano huu wa watani endapo Simba itashinda utasikia sasa
hakuna vurugu za chini chini kwa wanachama wote wa Simba ni kitu kimoja, hata
wale wazee waliochukizwa baada ya kutimuliwa na uongozi mpya nao pia shwari.
Lakini kinyume na hapo utasikia balaa lake, kwa upande wa
Yanga kule kuko kimya muda mrefu hasa baada ya wale wanachama waliokuwa
wanampinga mwenyekiti wao Yusuf Manji kwa kuj9ongezea mudea nao utawasikia
endapo Yanga imepoteza, watakuja na hoja yao ya kumng’oa kabisa kuwa Manji
hawafai Wanayanga na anaidhalilisha Yanga, Kikubwa wanachama hao watapata nguvu
kutoka kwa wanachama wengine waliochukizwa na kipigo toka kwa Simba, hapo ndipo
bomu linapolipuka.
Kitu kikubwa na cha muhimu ni
kusubiri kisha tuone, sina mengi sana wadau wangu isipokuwa tuombe mungu siku
ya siku ifike tushuhudie mpambano wa kihistoria, timu hizi msimu uliopita
hazikufungana kabisa, mechi zote mbili zilitoka sare, walianza katika mzunguko
wa kwanza ambapo walifungana 3-3 na mzunguko wa pili 1-1, 0652 626627