NYERERE DAY: TUMUENZI NYERERE KWA VITENDO
Ili kumuenzi Nyerere, TFF irejeshe kombe lake
Na Fikiri Salum
WATANZANIA wameadhimisha siku ya kumbukumbu ya kifo chake
rais wa kwanza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere
ambaye alifariki Oktoba 14 mwaka 1999 katika hospitali ya Mtakatifu Thomas
nchini Uingereza.
Ni miaka 15 tangia kifo chake ambapo kuna mengi ya kukumbuka
enzi za utawala wake, kumbukumbu ya Nyerere ndiyo imenisukuma hadi kuandika
makala hii, Watanzania wengi wamekuwa wakimzungumzia Mwalimu kutokana nay ale aliyofanya
ambapo wengi wao wanasema bado Watanzania wameshindwa kumuenzi kwa vitendo.
Inawezekana ni kweli Watanzania wameshindwa kumuenzi kwa
vitendo mwalimu Nyerere na hutumia magazeti na vyombo vingine vya habari
kumuenzi huku vitendo hakuna, rushwa imechukua nafasi ambapo sasa hivi
imeonekana kama fasheni, ukienda hospitali lazima utumie rushwa ili uhudumiwe
haraka.
Ipo hivyo hata polisi, lazima rushwa itumike ili kumtoa
ndugu yako aliyeshikiliwa au wewe mwenyewe, kama hivyo basi ataendelea kusota
rumande, mahakamani ambapo ndiko kunakoaminika kwa sheria lakini siku hizi nako
kumebadilika, ili kesi iende haraka itakugharimu utoe kitu kidogo.
Kusema kweli mambo siku hizi hayaendi ipasavyo na rushwa
imekuwa kama haki vile, katika makala yangu ya leo namzungumzia mwalimu Nyerere
ambaye muasisi wa taifa hili, Nyerere ni mmoja kati ya wanaharakati wa kwanza
nchini waliopigania uhuru wan chi hii.
Kutokuwepo kwake kumefanya jitihada kadhaa alizokuwa anazipigania
kukwama, Nyerere alipenda watu wake wawe na uhuru wa kweli baada ya kuupata
kutoka kwenye minyororo ya Wakoloni, Tanganyika baadaye Tanzania ilitawaliwa na
Wajerumani na baadaye Waingereza.
Nyerere alitumia mchezo wa soka ili kupigania uhuru wan chi hii,
pia alifanikisha muungano kati yetu na Zanzibar ambayo nayo ilikuwa katika
utawala wa kimabavu wa Sultan wa Oman na Waingereza, baada ya kuungana na kuwa
taifa moja Tanzania, Nyerere aliendelea kusaidia juhudi mbalimbali katika
michezo.
Enzi zake alihakikisha timu za taifa zinafanya vizuri na
kuwakilisha vema Tanzania na kweli ili9kuwa hivyo ambapo timu ya taifa ya
riadha ilifanya kweli katika mashindano ya Madola yaliyofanyika Scotland ambapo
mwanariadha Filbert Bayi alivunja rekodi ya dunia.
Haikuwa kwa Bayi peke yake isipokuwa wanariadha wengine kama
Seleman Nyambui, Juma Ikhangaa na wengineo walifanya kweli, Tanzania ilisifika
katika mchezo wa riadha kiasi kwamba majirani zetu Kenya walisubiri kwanza, lakini
sasa hivi Kenya iko mbele na Tanzania inasuasua.
Nyerere tutamkumbuka kwa mengi hasa pale alipoteua waziri wa
elimu na utamaduni ambaye alipigana kwa nguvu zote kuhakikisha Tanzania
inafanya kweli katika michezo, michezo ilishamili hadi mashuleni ambapo masomo
maalum ya michezo yalienziwa.
Katika harakati zake za kisiasa Nyerere hukuwa nyuma katika kupenda michezo hasa soka, TFF inapaswa kumuenzi
Mbali na michezo mashuleni kuenziwa, timu ya taifa ya mpira
wa miguu ya Tanzania ilikuwa miongoni mwa timu tishio barani Afrika, mwaka
1980, Taifa Stars ilifuzu fainali za mataifa huru barani Afrika (Mataifa
Afrika) iliyokuwa inafanyika nchini Nigeria.
Stars ilikwenda kushiriki fainali hizo zilizokuwa
zinashirikisha timu za mataifa manane tu tofauti na sasa mataifa 16
yanashiriki, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza Taifa Stars kushiriki fainali hizo
na pia ni mara ya mwisho, hadi sasa Stars haijashiriki fainali hizo zaidi zaidi
ilishiriki fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani
CHAN.
Nyerere tutaendelea kumkumbuka kutokana na juhudi zake
binafsi ambapo alianzisha vyama mbalimbali vya kusimamia michezo hapa nchini,
TFF zamani FAT iliasisiwa enzi za Nyerere hivyo ni moja kati ya zao lake,
katika taasisi hiyo kubwa nchini imeshindwa kumuenzi barabara.
TFF imeshindwa kuyarejesha mashindano yalikuwepo zamani ya
kombe la Nyerere ambayo yalikuwana hadhi kubwa, mashindano hayo ya mpira wa
miguu yalishirikisha timu zinazoshiriki ligi kuunamadaraja mengine ambapo
bingwa anapata tiketi ya kushiriki kombe la CAF sasa Shirikisho.
Nakumbuka michuano hiyo ilifanyika mara mbili ambapo timu ya
JKT Ruvu ya Pwani ndio ilikuwa mabingwa na ilipata nafasi ya kushiriki kombe la
Washindi barani Afrika lakini TFF wakati FAT ilishindwa kuwasilisha majina ya
wachezaji wake CAF na kufanya iondolewe katika michuano hiyo.
Baadaye Tanzania ilisimamishwa na CAF kutokana na kutopeleka
wawakilishi katika michuano ya CAF, uzembe huo ulifanyika na baadaye kombe la
Nyerere likashindwa kufanyika, kushindwa kufanyika kwa kombe la Nyerere kulitokana
na uzembe wa viongozi wa FAT.
Wakati sasa TFF inaongozwa na Jamal Malinzi ambaye wakati
akinadi kampeni zake za kuingia madarakani aliahidi kuyarejesha mashindano hayo
ya mwalimu Nyerere, Malinzi amefikisha mwaka mmoja tangia aingie TFF lakini
bado hajaweza kutimiza ahadi yake.
Ili kumuenzi Nyerere michuano yake yenye jina lake inapaswa
kurejeshwa ili kuenzi mema yake na mchango wake mkubwa alioutoa kwenye soka,
Kama Watanzania wanaamini kuwepo kwa viongozi wa dini siku timu ya taifa, Taifa
Stars inawafunga Benin pale kwenye uwanja wa Taifa mabao 4-1 basi uwepo wa
michuano ya Nyerere Cup kunaweza kuleta Baraka nyingine na kubwa kwenye soka la
nchi hii.
Jina la Nyerere limetapakaa kila mahari lakini michuano ya Nyerere Cup ndiyo pekee inaweza
kulienzi jina hilo, pia michuano ya Nyerere inazishirikisha timu kubwa na
kongwe hapa nchini kama Yanga na Simba hivyo inaweza kutumika kupatikana kwa
fedha ambazo zinaweza kuingia katika mfuko wake wa Nyerere Foundation.
Bado mwalimu Nyerere ni muhimu katika maendeleo ya soka letu
kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa, Nyerere alihakikisha klabu kongwe za
Simba na Yanga zinadumu katika soka la nchi hii, timu hizo zilitumika
kuunganisha umoja ambapo ndio sera kubwa ya mwalimu.
Simba na Yanga zilitumika kuhakikisha amani ya nchi hii
inaendelea kwani timu hizo zimekuwa na mashabiki wengi na nusu yake ni sawa na
theluthi mbili ya Watanzania wote, kuwepo kwa Simba na Yanga kumechangia kuwepo
kwa mshikamano baina ya Watanzania na majirani zao, timu hizo zimekuwa
zikishiriki mara kwa mara michuano ya klabu bingwa Afrikamashariki na kati.
Namkumbusha tena rais wa TFF
Jamal Malinzi kuyarejesha mashindano ya
kombe la Nyerere ili kumuenzi muasisi huyo wa taifa hili, Mwenyezi mungu
amuweke mahara pema peponi Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Burito
Wanzagi Nyerere, 0755 522216.