PELLE KUICHEZEA ITALIA KWA MARA YA KWANZA

Graziano Pelle 

Straika wa klabu cha ligi ya Premier ya Uingereza, Graziano Pelle anatarajiwa kuchezea taifa lake la kuzaliwa Italia kwa mara ya kwanza kwenye ngoma ya kufuzu Kombe la Euro la 2016 dhidi ya Malta.

Wana Azzurri wanalenga kushinda mechi ya tatu mtawalia katika Kundi H baada ya kukomesha Norway (2-0) na Azerbaijan (2-1) huku vijana wa Antonio Conte wakilaumiwa kwa kukosa nafasi nyingi mbele ya lango.
Washambuliaji Ciro Immobile (Borussia Dortmund) na Simone Zaza (Sassuolo) walialika gadhabu ya wengi kwa kutupa fursa nyingi dhidi ya Azerbaijan Ijumaa jijini Palermo na kocha huyo amekita matumaini yake na Pelle.


“Anaweza kuwa mchezaji muhimu kwetu kwani uwezo wake wa kutumia nguvu alizonazo za maumbile zitachangia pakubwa dhidi ya wapinzani wanaofurisha wachezaji kwenye ngome,” Conte aliambia RaiSport.

“Tunahitaji mchezaji anayeweza kumiliki mpira vizuri na kuruhusu wenzake waingie mchezoni,” aliongeza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA