MAXIMO AIKATIA TAMAA YANGA KWA SIMBA
Aidha, Mbrazil huyo amesema hana mpango wa kulipa kisasi cha kipigo cha mabao 5-0 ambacho Yanga ilikipata msimu wa 2011/12 dhidi ya Simba.
Akizungumza mara tu baada ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) waliyoshinda 2-1 dhidi ya JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi, Maximo alisema haihofii Simba na anaamini ataifunga katika mechi hiyo.
“Nimekaa Tanzania kwa muda mrefu, ninaijua Simba, ni timu nzuri na kubwa nchini. Uwezo wa kocha (Patrick) Phiri ni mkubwa, ni kocha mzuri na mzoefu wa mechi kama hiyo. Lakini kikosi changu kina
"Tumecheza mechi yenye upinzani mkali dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC lakini tuliwashinda na kutwaa Ngao ya Jamii. Ninafikiri hatupaswi kuwaogopa Simba ingawa tunatambua mechi itakuwa ngumu na yenye upinzani mkali," alisema.
Kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars alisema anatambua Simba wanahitaji kulinda heshima kwa kuifunga timu yake na pia kupata ushindi wa kwanza msimu huu ili kuwapa faraja mashabiki wao ambao wamekuwa wakiondoka vichwa chini uwanjani tangu kuanza kwa VPL msimu huu.
"Itakuwa mechi ngumu kwa sababu inakutanisha timu kubwa zenye mashabiki wengi nchini, lakini tunapaswa kukiamini kikosi chetu," alisema zaidi Maximo.
Kuhusu kiu ya Yanga kulipa kisasi cha 5-0, Maximo alisema: "Hii ni ligi, tunachohitaji ni ushindi tu, siyo kushinda idadi kubwa ya mabao na kulipa kisasi. Muhimu kwa sasa ni kupata pointi tatu katika kila mechi,” alisema.
Baada ya kupigwa 2-0 dhidi ya mabingwa mara mbili wa Tanzania Bara 1999 na mwaka wa mabadiliko ya karne, Yanga chini ya Maximo imeshinda mechi mbili mfululizo ikianza na 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons lakini katika mechi zote tatu imeruhusu nyavu zake kutikishwa.
Maximo aliyeanza kuinoa Yanga msimu huu akirithi mikoba ya Mholanzi Hans va Der Pluijm, akiongoza Yanga katika mechi nane, akishinda saba na kupoteza moja atakutana na Kikosi cha Simba ambacho kimepata sare tatu katika mechi zote tatu za mwanzo za VPL msimu huu.
MAXIMO YANGA
Yanga 1-0 Chipukizi (kirafiki, Pemba)
Yanga 2-0 Shangani (kirafiki, Zanzibar)
Yanga 2-0 KMKM (Kirafiki, Zanzibar)
Yanga 1-0 Thika United (Kirafiki Taifa)
Yanga 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
Mtibwa 2-0 Yanga (VPL)
Yanga 2-1 Prisons (VPL)
Yanga 2-1 JKT Ruvu (VPL)
wachezaji wazoefu pia," alitamba Maximo.