OKWI AJIFUNGA MIAKA MIWILI SIMBA
Kiungo mshambuliaji wa
Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, ameongeza mkataba wa kuichezea timu hiyo akisaini miaka miwili.
Awali, kiungo huyo mwenye
kasi kubwa uwanjani, alisaini mkataba wa miezi sita ya kuichezea timu hiyo akitokea
Yanga, akiondoka kwa mgogoro mkubwa.
Meneja wa kiungo huyo, Abdulfatah Saleh,alisema
kuwa Okwi ameongeza mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya pande mbili
kati yao na klabu hiyo.
Abdulfatah alisema, awali
kiungo huyo alisaini mkataba mfupi wa kuichezea Simba ili kupisha kesi
iliyopo kati yake (Okwi) na Yangailiyomfungulia mashtaka kwa madai ya kukiuka makubaliano
yaliyokuwepo kwenye mkataba.
Aliongeza kuwa, mara
baada ya kumalizika kwa kesi hiyo iliyosimamiwa na Kamati yaSheria, Maadili na Hadhi za
Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ndiyo akaongeza mkataba huo
mwingine.
“Okwi ameongeza mkataba
mwingine wa kuichezea Simba, amesaini mkataba wa miaka miwili baada ya kesi
yake na Yanga kumalizika kwa TFF kumruhusu kuichezea Simba kufuatia timu ya
zamani kushindwa kutimiza makubaliano yaliyokuwepo kwenye mkataba wake.
“Mwanzoni
alisaini mkataba wa miezi sita ili kupisha kesi hiyo imalizike, awali alisaini
mkataba huo kwa hofu ya kushindwa kesi hiyodhidi ya Yanga,” alisema Abdulfatah.