KOCHA ENGLAND AKOMSOA RODGERS

Kocha wa England Roy Hodgson amehoji kauli ya kocha wa Liverpool Brenden Rodgers ya kwamba wachezaji wanahitaji siku mbili baada ya mechi ili kuwawezesha kurejea katika hali zao za kawaida.
Kauli ya kocha huyo wa Liverpool ilikuja baada ya mchezaji Raheem Sterling kulalamika kuchoka kabla ya mchezo wa ugenini wa England mchezo ambao timu hiyo iliibuka kidedea dhidi ya Estonia.


'Raheem anaweza kusema kwamba kitu Fulani kinakuwa kinajitokeza kwake na alihisi kuhitaji kusema kuhusu kuwa mchovu kuliko kunyamaza' alisema Hodgson.

'Sidhani kama kuna ushahidi wa kitabibu kusaidia kauli ya siku mbili za kurejea katika hali ya kawaida' aliongeza kocha huyo.

Uhusiano kati ya Roy Hodgson na Brenden Rodgers ulikuwa tayari umezorota baada ya mchezaji Daniel Sturridge kupata majeraha katika majukumu ya timu ya Taifa mwanzoni mwa mwezi September.
Rodgers alikasirika pindi Sturridge alipopata nmaumivu ya paja mazoezini baada ya ushindi wa England wa bao 1-0 dhidi ya Norway huku kocha huyo akisisitiza kuwa wachezaji wenye kasi wanahitaji kupumzika.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA