ZAMBIA YAMPATA KOCHA MPYA

Timu ya soka ya Zambia imemuajiri Nico Lobohm kama naibu kocha wa Honour Janza.

Raia huyo wa Uholanzi amepewa kandarasi kuwa miongoni mwa kamati ya kiufundi hadi mwisho wa kampeni ya kuwania kufuzu katika kombe la mataifa bingwa barani afrika mnamo mwaka 2015.

Rais wa Shrikisho la soka nchini Zambia Kalusha Bwalya amebaini kuwa Lobohom aliwahi kufanya kazi nchini humo.


''Ilikuwa vyema kwa sisi kumtafuta mtu ambaye anaelewa hali ya taifa hili, mtu ambaye anaweza kumsaidia mkufunzi Honour Janza'', alisema Bwalya.''Pengine Lobohm atabakia,

Nadhani atapendelea kandarasi hiyo na kufanya kazi hapa nchini'', alisema Bwalya.

Bwalya amesema kuwa Kocha huyo ataleta maarifa mengi na ni hicho ndicho wanachotaka.

Kocha huyo amekuwa nchini humo kwa mda mrefu ,amefanya kazi Uholanzi,Hong Kong,Surinam,Tunisia na Zambia.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA