BADO NAIHESHIMU ARSENAL- FABREGAS

Cesc Fabregas

Nahodha wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas, ambaye alingaria maadui wao Chelsea kwenye ngoma kali ya ligi ya Premier Jumapili, amesema bado anaheshimu waajiri wake wa zamani licha ya mashabiki wao kumkemea.

Fabregas alimwandalia Digo Costa pasi ya juu juu iliyomwezesha kufunga goli la pili kunyamazisha Arsenal 2-0 katika uga wa Stamford Bridge na alitajwa kama mchezaji bora zaidi wa mechi hiyo baadaye.

"Naheshimu Arsenal sana kwani walipatia fursa kubwa nikiwa chipukizi na bila wao, seingelikuwa hapa au kushinda mataji.

“Najua wananipenda licha ya kejeli zao na ni kwasababu tulikuwa pamoja wakati mmoja. Lakini matukio wakati mwingine yanaongoza yale yalitendeka na ni hali ya mchezo,” kiungo huyo wa
Uhispania alisema.

“Alicheza mchezo wa kuvutia sana na kumpa haki yake, hakufanya bidii za ziada kwasababu Arsenal ndio walikuwa wapinzani wetu ila amekuwa kwatika hali hiyo tangu aje hapa,” mwalimu wake Jose Mourinho alimsifu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA