YANGA WAANZA KUINGIWA NA KIWEWE MECHI YA SIMBA, YONDANI, CANNAVARO HATIHATI KUCHEZA

Wanachama na wapenzi wa Yanga SC wameendelea kuilaumu TFF inayoongozwa na rais Jamal Malinzi kwa kitendo chao cha kuihujumu kuelekea mchezo wa watani wa jadi jumamosi.

Wanachama hao wa Yanga wamelia na TFF kwa kitendo chao cha kuahirisha mchezo wao dhidi ya Simba SC ambao ulikuwa uchezwe Oktoba 12 ili kupisha timu ya taifa, Taifa Stars iliyocheza na Benin. Wameendelea kusema kuwa kusogezwa kwa mechi yao na kuipisha timu ya taifa ilikuwa mbinu ya kuihujumu Yanga kwani kalenda ya Fifa ilikuwa wazi kabla hata ratiba ya ligi ya kuu haijatoka.


'Inatushangaza sana kwani timu ya taifa imesababisha wachezaji wetu Kelvin Yondani na Nadir Haroub 'Cannavaro' kuumia', walisema.

Yondani na Cannavaro waliumia katika mchezo huo ulioishia kwa Taifa Stars kuifunga Benin 4-1 katika mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na Fifa. Yanga iko shakani kuwakosa nyota hao dhidi ya Simba na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wake.

Simba nao wameanza kupata nafuu kufuatia majeruhi wake wote kurejea uwanjani isipokuwa Paul Kiongera ambaye kwa mujibu wa daktari bado ataendelea kukaa nje ya uwanja kwakua ana maumivu makubwa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA