Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2026

Hasheem Thabit achaguliwa kuwa Rais wa TBF

Nyota wa basketball Tanzania, Hasheem Thabeet amechaguliwa kuwa rais wa chama cha mpira wa kikapu Tanzania (TBF) baada ya kushinda kinyanganyiro hicho katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Dodoma. Katika uchaguzi huo Hasheem ameibuka mshindi baada ya kupata kura 34 kati ya 60 zilizopigwa na wajumbe wote. Hashem kwa sasa anachezea timu ya kikapu ya Dar City ambayo inatarajiwa kucheza fainali za ‘BAL’ kwenye michezo itakayochezwa kuanzia Machi 27 nchini Afrika Kusini. Wengine walioshinda katika uchaguzi huo Mohamed Kisui (Makamu wa Rais), Mwenze Fiston Kabinda (Katibu Mkuu) na Simon Milondo (Naibu Katibu Mkuu).

Yanga wapiga tizi la mwisho la kuivaa Simba kesho

Kikosi cha Yanga SC leo kimefanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuwavaa watani zao Simba SC kesho mchezo wa Ligi Kuu bara katika uwanja wa New Amaan Stadium, Zanzibar.

Sebastian Nkoma: Ni kocha wa soka la wanawake aliyeinua vipaji hapa Tanzania

Na Abdul Makambo KOCHA Sebastian Nkoma ni mmoja wa makocha wazawa waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka hapa nchini Tanzania .Pamoja na nchi yetu wamepita makocha wengi wazawa wenye uwezo na majina makubwa kama Mansour Magram, Joel Bendera, Ray Gama, Ayoub Mohamed, Zacharia Kinanda na Elijah Kategile. Wengine ni Iddi Machupa, Pius Nyamko, Edmund Thomas, Mohamed Msomali, Salum Madadi, Abdalah Kibaden, Omary Mahadhi, Abdurahman Juma, Athuman Juma Kalomba, Silylelsaid Mziray, Kenny Mwaisabula, Hamim Mawazo na hao ni baadhi. Nkoma alipokuwa Yanga Princess (kulia) Nkoma ni mmoja wa makocha wetu wazawa mwenye moyo  Nkoma amezifundisha timu nyingi hapa Tanzania na baadhi ni kama Rhino ya Tabora. Soka la wanawake ndio lililomtoa kocha huyo, lakini kwa wanaume pia alianza kufanya mabalaa kwani aliifundisha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania yeye na Bakari Shime aliipeleka katika AFCON ndogo kule nchini Gabon, akiwa na wanasoka vijana kama Ramadhan Kabwili, Kibwana Shomari, Dickson J...

Barker aahidi ushindi dhidi ya Yanga kesho

Kocha wa Simba SC Steve Barker anasema wanayo fursa ya kubadili taswira yao kesho mbele ya watani wao Yanga. Ni mkutano wa makocha na manahodha wa Yanga na Simba

Pedro akiri Simba ni timu kubwa

Kocha wa Yanga SC, Pedro Goncalves anasema tangu ametua Jangwani wamecheza mechi kadhaa kubwa, lakini kesho wanakwenda kukutana na mpinzani wao mkuu. Ni mkutano wa makocha na manahodha wa Yanga na Simba 

Karia ampiga mkwara mwamuzi wa dabi

Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa Mwamuzi atakaeharibu mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC atafunguliwa mashitaka mahakamani na kuondolewa kwenye Mpira kabisa "Atakaejaribu kuharibu huo mchezo, sio tu kwamba ataondoka kwenye Mpira maisha yake yote pia tutamfungulia mashitaka kumshitaki, tumfunge wala hatutakuwa na masihara na hilo nalizungumza wazi" Rais Karia ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa 20 wa Mwaka wa TFF unaofanyika Leo Kahama.

Motsepe kuwania Urais Afrika Kusini

Bilionea wa Afrika Kusini, Patrice Motsepe, ameibuka katikati ya tetesi za uwezekano wa kugombea urais wa chama tawala cha African National Congress (ANC), licha ya yeye mwenyewe kukanusha mipango hiyo. Tetesi hizo zimeongezeka baada ya Motsepe kutangaza kustaafu nafasi yake ya mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya madini ya African Rainbow Minerals, hatua iliyotafsiriwa na baadhi ya wachambuzi kama dalili ya mwelekeo mpya wa kisiasa. Baadhi ya wanachama wa ANC wanaamini uzoefu wake wa kibiashara unaweza kusaidia kukuza sekta ya viwanda na kupunguza ukosefu wa ajira nchini South Africa. Hata hivyo, iwapo angechaguliwa, Motsepe angekuwa kiongozi wa kwanza wa ANC katika enzi ya demokrasia asiye na historia ya mapambano ya moja kwa moja dhidi ya ubaguzi wa rangi au kifungo cha kisiasa

Pyramids kuibomoa Al Ahly

Klabu ya Pyramids inaangalia uwezekano wa kumrudisha nchini Misri mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Al Ahly,Wessam Abou Ali. Abou Ali kwasasa anacheza ligi kuu nchini Marekani, inaelezwa ni endapo mshambuliaji hatari raia wa DRC, Fiston Kalala Mayele akitaka kuondoka,kuna uwezekano wa kumvuta Abou Ali. Inasadikika kiasi cha billion 39 za kitanzania kimewekwa na mabwenyenye wa klabu hiyo.. Wakati Abou Ali anaondoka Al Ahly, aliwahi kunukuliwa akisema,kama ni kurudi nchini Misri kucheza tena mpira basi hakuna timu nyingine ataichagua zaidi ya Al Ahly.

Khalid Aucho akana kujihusisha na utovu wa nidhamu

KIUNGO wa Kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho amesema kwenye maisha yake ya soka hajawahi kuhusishwa na utovu wa nidhamu kwa namna yoyote. Aucho ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kufuatia taarifa ya klabu ya klabu yake, Singida Bkack Stars kumsimamisha yeye na kipa Mnigeria, Amas Daniel Obasogie kwa tuhuma za utovu wa nidhamu. “Nimekuwa nikizingatia taaluma yangu kila wakati katika taaluma yangu, nikiiwakilisha kila klabu kwa heshima na nidhamu. Katika miaka yangu yote katika soka, sijawahi kuhusika katika kesi yoyote ya utovu wa nidhamu kwa sababu ninaelewa jukumu linalokuja na kuwa mchezaji mwadilifu. Kwa mashabiki wangu wapendwa ambao wamekuwa wakiniunga mkono kila wakati, hali litapita. Asante kwa msaada wako unaoendelea,” amesema mchezaji huyo wa zamani wa Yanga.

Ally Kamwe aihofia Simba

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe, ametoa kauli ya kushtua na ya kiungwana kuelekea mahasimu wao, Simba SC, akieleza kuwa amekuwa akifuatilia michezo yao kwa ukaribu ili kujifunza vitu mbalimbali. Kamwe amekiri kuwa Simba wamefanya usajili mzuri katika dirisha dogo la usajili, akilinganisha na daraja ambalo klabu hiyo ipo kwa sasa katika ramani ya soka. ​Katika kile kinachoonekana kama kutuliza presha ya mashabiki, Ally Kamwe amesisitiza kuwa mchezo wa hivi karibuni wa Simba haukuwa mbaya kama ambavyo watu wengi wanautafsiri. "Jana nilisema, watu wanaona kama utani ila kimsingi mechi yao ya juzi walicheza vizuri, walikosa bahati tu," alisema Kamwe, akionyesha utofauti na kauli za kashfa zinazoweza kutolewa na upande mwingine katika kipindi hiki cha ushindani mkali wa ligi.

Dudubaya awashukuru mashabiki wake baada ya upasuaji India

Mwanamuziki mkomgwe wa muziki wa kizazi kipya, Bongofleva, Godfrey Tumaini "Dudubaya" ametoka salama katika chumba cha upasuaji huko Delhi, India amesema kwasasa anaendelea vizuri. Dudubaya amefanyiwa upasuaji wa kuweka sawa pingili za mgongo, mwanamuziki huyo mkongwe amemshukuru Mungu, madaktari, mashabiki wake na wote wanaomtakia mema. Dudubaya amepelekwa India kufanyiwa upasuaji wa pingili na mpenzi wake Wastara Ili amuoe.

Sowah awajia juu wanaomchafua

Mshambuliaji wa Simba SC Jonathan Sowah amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu sakata linaloendelea kati ya yeye na timu hiyo lililopelekea kuondolewa kwake kambini kuelekea mchezo muhimu dhidi ya Yanga SC. "Sijajua kwanini nimeambiwa natakiwa kurudi Dar. Alinifuata meneja wa timu akanip ujumbe huo. Kwa kuwa ni kiongozi wangu sikutakiwa kumhoji sana zaidi ya kutekeleza." "Kuhusu madai ya utovu wa nidhamu, nasikia kutoka kwako lakini pia nimeona watu wanaandika tu kwenye mitandao ya kijamii. Nimesoma, ila nasubiri kwanza hicho kikao cha uongozi kujua sababu." "Nikimalizana na uongozi ndio nitawarudia hao ambao wameandika vitu bila kujua ukweli kutoka kwangu. Mimi sio mtu wa kukubali jina langu kuchafuliwa kirahisi."

Taasisi ya MO Dewji na Simba zatoa misaada kituo cha watoto yatima Zanzibar

Kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji, tumetoa msaada kwenye kituo cha Kutunza Watoto Yatima cha Mazizini kilichopo hapa Zanzibar, lakini pia tutapata futari pamoja leo jioni.

Bingwa wa Ligi ya mabingwa Afrika kupewa Dola milioni 6

Shirikisho la soka Afrika (CAF), limetangaza ongezeko la fedha za zawadi zinazotolewa kwa mshindi na mshindi wa pili katika Mashindano yake ya Vilabu, kuanzia msimu wa sasa wa 2025/2026. Chini ya muundo huo mpya wa zawadi, Mshindi wa Ligi ya Mabingwa wa CAF watapata Dola Milioni 6 ( Shilingi Bilioni 15.6 za Tanzania) huku Mshindi wa pili akijinyakulia Fola Milioni 2 (Shilingi Bilioni 5.2 za Tanzania). Timu zilizofika nusu fainali zitapata Dola Milioni 1.2 kila mmoja, na dola 900,000 kwa timu zilizotolewa katika robo fainali, na Dola 700,000 kwa vilabu vinavyomaliza nafasi ya tatu na nne katika hatua ya makundi. Kamati ya utendaji pia iliidhinisha pesa za juu zaidi kwenye Kombe la Shirikisho la CAF ambapo bingwa atatunukiwa Dola Milioni 4 (Shilingi Bilioni 10.4 za Tanzania) wakati Mshindi wa pili akitapata Dola Milioni 1 (Shilingi Bilioni 2.6 za Tanzania).

Rais Wallace Karia atembelea mradi wa Barrick Tanzania, Buzwagi

Rais wa TFF Wallace Karia akiongozana na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji TFF na Katibu Tawala Wilaya ya Kahama Glory Absalum leo wametembelea Mradi wa ufungwaji wa Barrick Tanzania, Buzwagi uliopo Kahama, Shinyanga kutazama miundombinu iliyopo kwa ajili ya kuanzisha Kituo cha Soka kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu