Shirikisho la soka Afrika (CAF), limetangaza ongezeko la fedha za zawadi zinazotolewa kwa mshindi na mshindi wa pili katika Mashindano yake ya Vilabu, kuanzia msimu wa sasa wa 2025/2026.
Chini ya muundo huo mpya wa zawadi, Mshindi wa Ligi ya Mabingwa wa CAF watapata Dola Milioni 6 ( Shilingi Bilioni 15.6 za Tanzania) huku Mshindi wa pili akijinyakulia Fola Milioni 2 (Shilingi Bilioni 5.2 za Tanzania).
Timu zilizofika nusu fainali zitapata Dola Milioni 1.2 kila mmoja, na dola 900,000 kwa timu zilizotolewa katika robo fainali, na Dola 700,000 kwa vilabu vinavyomaliza nafasi ya tatu na nne katika hatua ya makundi.
Kamati ya utendaji pia iliidhinisha pesa za juu zaidi kwenye Kombe la Shirikisho la CAF ambapo bingwa atatunukiwa Dola Milioni 4 (Shilingi Bilioni 10.4 za Tanzania) wakati Mshindi wa pili akitapata Dola Milioni 1 (Shilingi Bilioni 2.6 za Tanzania).
