Karia ampiga mkwara mwamuzi wa dabi

Rais wa TFF Wallace Karia amesema kuwa Mwamuzi atakaeharibu mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC dhidi ya Simba SC atafunguliwa mashitaka mahakamani na kuondolewa kwenye Mpira kabisa

"Atakaejaribu kuharibu huo mchezo, sio tu kwamba ataondoka kwenye Mpira maisha yake yote pia tutamfungulia mashitaka kumshitaki, tumfunge wala hatutakuwa na masihara na hilo nalizungumza wazi"

Rais Karia ameyasema hayo leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa 20 wa Mwaka wa TFF unaofanyika Leo Kahama.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI