Na Abdul Makambo
KOCHA Sebastian Nkoma ni mmoja wa makocha wazawa waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo ya soka hapa nchini Tanzania
.Pamoja na nchi yetu wamepita makocha wengi wazawa wenye uwezo na majina makubwa kama Mansour Magram, Joel Bendera, Ray Gama, Ayoub Mohamed, Zacharia Kinanda na Elijah Kategile.
Wengine ni Iddi Machupa, Pius Nyamko, Edmund Thomas, Mohamed Msomali, Salum Madadi, Abdalah Kibaden, Omary Mahadhi, Abdurahman Juma, Athuman Juma Kalomba, Silylelsaid Mziray, Kenny Mwaisabula, Hamim Mawazo na hao ni baadhi.
Nkoma ni mmoja wa makocha wetu wazawa mwenye moyo Nkoma amezifundisha timu nyingi hapa Tanzania na baadhi ni kama Rhino ya Tabora.
Soka la wanawake ndio lililomtoa kocha huyo, lakini kwa wanaume pia alianza kufanya mabalaa kwani aliifundisha timu ya taifa ya vijana ya Tanzania yeye na Bakari Shime aliipeleka katika AFCON ndogo kule nchini Gabon, akiwa na wanasoka vijana kama Ramadhan Kabwili, Kibwana Shomari, Dickson Job, Nickson Kibabage, Yohana Nkomola, Israel Mwenda na hao wote ni matunda yake.
Kocha Nkoma ni mtu serius anapokua kazini mara nyingi anampenda mchezaji mwenye displin uwanjani kama huna displin hata ukiwa staa na jina kubwa anakuweka pembeni niseme kocha Nkoma ni mtu mwenye msimamo na anaezingatia nidhamu.
Kuna kipindi kocha Abdelhak Benchika alivyoondoka katika klabu ya Simba SC akaletwa kocha Juma Mgunda na Sebastian Nkoma wakaenda Malawi , Simba ikicheza na Bata Bulleti na wakaenda nchini Angola.
Pia kiungo wa JKT Tanzania, Ally Msengi amepita kwenye mikono yake, ipo haja kwa TFF na serikali ikawaangalia kwa jicho pana makocha wazawa kutokana na mchango katika nchi nao wawe sehemu katika benchi la ufundi la timu ya taifa, Taifa Stars.
Sebastian Nkoma pia amewahi kuzifundisha timu za wanawake za simba Queens na Yanga Princess kwa nyakati tofauti.
Na akiwa Simba Queens amewahi kushinda ubingwa wa Ligi Kuu bara ingawa alipoenda Yanga Princess hakufanikiwa kutwaa ubingwa, kwa sasa kocha huyo hana timu yoyote hivyo milango Iko wazi kwa timu yoyote kumchukua.
Bila shaka wasomaji wetu wa mambo uwanjani mumemfahamu alieibua vipaji vya soka.

