Ally Kamwe aihofia Simba

Afisa Habari wa Young Africans, Ally Kamwe, ametoa kauli ya kushtua na ya kiungwana kuelekea mahasimu wao, Simba SC, akieleza kuwa amekuwa akifuatilia michezo yao kwa ukaribu ili kujifunza vitu mbalimbali.

Kamwe amekiri kuwa Simba wamefanya usajili mzuri katika dirisha dogo la usajili, akilinganisha na daraja ambalo klabu hiyo ipo kwa sasa katika ramani ya soka.

​Katika kile kinachoonekana kama kutuliza presha ya mashabiki, Ally Kamwe amesisitiza kuwa mchezo wa hivi karibuni wa Simba haukuwa mbaya kama ambavyo watu wengi wanautafsiri.

"Jana nilisema, watu wanaona kama utani ila kimsingi mechi yao ya juzi walicheza vizuri, walikosa bahati tu," alisema Kamwe, akionyesha utofauti na kauli za kashfa zinazoweza kutolewa na upande mwingine katika kipindi hiki cha ushindani mkali wa ligi.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI