Mshambuliaji wa Simba SC Jonathan Sowah amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu sakata linaloendelea kati ya yeye na timu hiyo lililopelekea kuondolewa kwake kambini kuelekea mchezo muhimu dhidi ya Yanga SC.
"Sijajua kwanini nimeambiwa natakiwa kurudi Dar. Alinifuata meneja wa timu akanip ujumbe huo. Kwa kuwa ni kiongozi wangu sikutakiwa kumhoji sana zaidi ya kutekeleza."
"Kuhusu madai ya utovu wa nidhamu, nasikia kutoka kwako lakini pia nimeona watu wanaandika tu kwenye mitandao ya kijamii. Nimesoma, ila nasubiri kwanza hicho kikao cha uongozi kujua sababu."
"Nikimalizana na uongozi ndio nitawarudia hao ambao wameandika vitu bila kujua ukweli kutoka kwangu. Mimi sio mtu wa kukubali jina langu kuchafuliwa kirahisi."
