HATUTAFANYA HAMASA- AHMED ALLY
Meneja wa Habari wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabuvyake haitafanya hamasa kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Power Dynamos kwakuwa uwanja utaingiza watu wachache.
Ahmed Ally amedai wataitumia mechi hiyo kama sehemu ya maandalizi ya kujiandaa na michuano ya African Football League itakayoanza hivi karibuni.
"Hatutafanya hamasa kubwa maana tunaweza kuwatia watu mzuka alafu tutakosa sehemu ya kuwaweka, itakuwa ya kawaida sababu watu 7,000 tutajaza kwa haraka."
"Mechi hii tutaitumia kama maandalizi ya kwenda kucheza CAF Football League."- Ahmed Ally.