YANGA HAOOO MAKUNDI

Na Fikiri Salum

MABINGWA wa soka Tanzania bara, Dar Young Africans, maarufu Yanga SC usiku wa leo imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa Afrika, baada ya kuichapa bao 1-0 timu ya El Merreikh ya Sudan katika uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 

Kwa ushindi huo Yanga SC inatinga moja kwa moja hatua ya makundi, hasa baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-0.

Yanga ilitangulia kushinda kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Pele mjini Kigali nchini Rwanda. 

Goli pekee la Yanga lilifungwa na Walid Clement Mzize, kesho wawakilishi wengine wa Tanzania Simba SC watawakaribisha Power Dynamos katika uwanja huo huo wa Azam


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA