RAINFORD KALABA AISAPOTI POWER DYNAMOS

Gwiji wa Chipolopolo na TP Mazembe Rainford Kalaba ameiunga mkono Power Dynamos kuifunga Simba SC ya Tanzania wikendi hii katika mchezo wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika wikendi hii.

Ikumbukwe Kuwa Dynamos ina mlima mkubwa wa kupanda baada ya kutoka sare ya 2-2 nyumbani katika mechi ya kwanza. Walifunga Goli La Kwanza kupitia kwa Joshua Mutale na Cephas Mulombwa, lakini juhudi zao zikazimwa na Clatous Chama, aliyefunga mabao yote Mawili Ya kusawazisha

Huku kukiwa na uchezaji mkali unaohitajika ili kusonga mbele kwa raundi zinazofuata, Kalaba anaiambia Duniayetu kwamba bado haijakamilika kwa Aba Yellow.

"Wasahau Kuhusu Matokeo Ya Kwanza, Wachukulie Kama Zile ni Dakika 45 Za Kipindi Cha Kwanza, Na Ni rahisi Power Dynamos Kuwafunga Simba sc Pale Tanzania Kuliko Simba Sc Kuwafunga Yeah Maana Wao Watakuwa Na Presha Kubwa Mbele Ya Mashabiki Wao" Alisema Rainford Kalaba

Aliongeza Na Kusema "Katika Mpira Lolote Linawezekana, Na Hakuna Timu Isiyofungika na Kama Mliwafunga goli 2 Mchezo Wa Kwanza Basi Mnaweza Kuwafunga Zaidi Ya Goli 2 maana Tayari Mnawajua Wapi Wako bora na wapi Wanaudhaifu"


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA