DUBE KUIKOSA YANGA
Klabu ya Azam FC imetangaza kuwa Mshambuliaji wao hatari,Prince Dube anatarajiwa kukaa nje ya Uwanja kwa mda wa wiki tatu kufuatia kupata majeraha ya nyonga kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo Azam ilikutana na Singida Fountain Gate FC.
Kwenye mda ambao atakuwa nje Prince Dube atakosa mechi mbili za Ligi Kuu ambazo zitakuwa ni dhidi ya Dodoma Jiji pamoja na Coastal Union na huku kama akopona mapema huenda akarudi Uwanjani kwenye mechi kati ya Azam FC dhidi ya Yanga ambayo itakuwa October 25 ikiwa ni siku nne tangu mda ambao amepangiwa na Daktari wa kukaa nje ya Uwanja kuisha.
Pia Azam FC imetangaza kuwa Kiungo Mshambuliaji wao,Yahya Zaidi Pia atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki tatu kufuatia kuchanika kwa Kiraba (meniscus) kinachokuwa katikati ya goti, kinacholiimarisha lisikwaruzane.
Kiraba hicho pia huwezesha goti kufanya kazi vizuri kwa maana ya kukunja na kukunjua.