SIMBA KUCHEZA SAA 10 NA POWER DYNAMOS

"Mchezo dhidi ya Power Dynamos utachezwa siku ya Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Tumeamua kucheza saa 10 sababu michezo mingi hapa karibuni tumecheza muda huo hivyo hatukutaka kubadili muda lakini pia Jumatatu itakuwa siku ya kazi hivyo tunataka watu wawahi kurudi nyumbani."

"Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio utafatiliwa zaidi Afrika kwa wikiendi hii kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Ukubwa wa Simba SC ndio unafanya mchezo huo uwe mkubwa zaidi."

"Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui."

"Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo."- Ahmed Ally.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA