YANGA KUENDELEZA 5G KESHO?
Kikosi cha wachezaji wa wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga SC leo wameendelea kujifua wakijiandaa kucheza kesho na wawakilishi wa Sudan,El Merreikh katika uwanja wa Azam Complex, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Yanga inahitaji sare yoyote au kufungwa goli moja ili iweze kusonga mbele kwani mpaka sasa ina ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata Kigali, Rwanda katika mchezo wa mkondo wa kwanza ambapo El Merreikh ilikuwa nyumbani.