Machapisho

Siri zavuja, Kessy aibwaga Simba

Picha
Na Mwandishi Wetu Dalili za beki Hassan Ramadhan Kessy kukipiga Yanga bila vikwazo huenda ikafanikiwa baada ya kamati iliyoketi hivi karibuni iliyoongozwa na wakili Richard Sinamtwa kuitaka Klabu ya Simba kuwasilisha vielelezo kama imewahi kumlipa beki huyo mshahara wake wa miezi mitatu kupitia akaunti yake ya benki. Endapo Simba itashindwa kuwasilisha vielelezo hivyo basi beki huyo atakuwa ameibwaga Klabu yake hiyo ya zamani kwani kesi hiyo itatupiliwa mbali. Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa ndiye aliyeiomba kamati hiyo kuhoji kama ni kweli Simba walikuwa na uhalali wa kummiliki mchezaji huyo, hata hivyo kesi hiyo bado inapigwa danadana

Wakala wa Jesse Were awaita mezani Yanga

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Wakala wa mshambuliaji wa timu ya Zesco United ya Zambia Jesse Were raia wa Kenya, George Bwana amesema mchezaji wake yuko sokoni na anamuuza kwa kiasi kisichopungua Dola 150,000 sawa na shilingi Milioni 320 za Kitanzania. Bwana amewaambia Yanga kuweka mezani kitita hicho ili straika huyo atue Jangwani, Were ni chaguo la kocha mpya wa Yanga, Mzambia George Lwandamina. Tayari Yanga imeshamshusha kiungo mkata umeme wa Zesco United ya Zambia, Justin Zullu ambaye muda wowote atamwaga wino kuitumikia Klabu hiyo

Rage ampiga kijembe Malinzi

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Aliyekuwa mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Alhaj Ismail Aden Rage amempiga kijembe Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi kwambs si mtu wa mpira na ndio maana katika utawala wake tunashuhudia Tanzania ikiporomoka katika viwango vya ubora huku hali ikizidi kuwa mbaya. Rage amesema viongozi wa sasa wengine walikuwa wanaongoza masumbwi na anashangaa kuwaona wakiliongozs soka. Malinzi ndiye aliyekuwa akiongoza masumbwi, enzi zake akimpromoti bondia Rashid Matumla kupitia kampuni yake ya DJB Promotion. Kwa sasa Malinzi ameshindwa kuivusha Tanzania kwani timu zake zote za Taifa zimetolewa kwenye mashindano iliyoshiriki, pia tumeshuhudia Tanzania ikianguka kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA), Tanzania kwa sasa inashika nafasi ya 160 ikiwa ni nafasi mbaya kabisa kuwahi kushjka

Bokungu kuongezwa miezi sita Simba

Picha
Na Salum Fikiri Jr  Dar es Salaam Klabu ya Simba imesema itamuongezea mkataba wa mwingine wa miezi sita, beki wake wa kulia Janviel Besala Bokungu raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Bokungu atapewa mkataba huo mara baada ya kumalizika kwa huu mwingine wa miezi sita, Tayari Simba imeshamuongezea beki wake wa kushoto Mohamed Hussein 'Tshabalala' wa miaka miwili. Bokungu aliyesajiliwa sambamba na Mkongo mwenzake Musa Ndusha, ameonyesha kiwango kikubwa katoka michezo kadhaa ambayo klabu yake ya Simba imecheza, endapo atapewa miezi sita, atalazimika kucheza hadi mwakani

Lwandamina ambakiza Mwambusi Yanga, Akana kuwaleta nyota wa Zesco Jangwani

Picha
Na Enika Samson, Dar es Salaam Kocha mpya wa Yanga SC  Mzambia George Lwandamina ambaye leo ametambulishwa na uongozi wa Klabu hiyo amesema atafanya kazi na benchi la ufundi alilolikuta. Ina maana kocha huyo wa zamani wa Zesco United ataendelea kufanya kazi na Juma Mwambusi ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga aliyefanya kazi na aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga, Hans Pluijm ambaye leo hii ametambulishwa kama Mkurugenzi wa Ufundi wa timu hiyo. Lwandamina pia amekanusha uvumi ulioenezwa na mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari kwamba aliwapendekeza nyota wawili wa Zesco United, Jesse Were raia wa Kenya na Meshark Chaila

Genge la RNE lapata mkataba mnono wa kutangaza Condom

Picha
Na Ismail Mhina, Tanga Kundi la muziki wa kizazi kipya lililopo Hale jijini Tanga, liko mbioni kuingia mkataba na moja kati ya makampuni makubwa ya kusambaza Condom hapa nchini. Mmoja wa mamemba wa kundi hilo linalotamba kwa sasa katika miondoko ya Hip Hop jijini Tanga, amesema wako mbioni kusaini mkataba huo mnono nankampuni hiyo ya kusambaza Condom. Kundi hilo linaloindwa na wasanii sita, wakiwemo Jusa, Amour JJ, Dizonga, Jimmy Msauzi, Boss Rapa, Agga Swing na Mkola Man Miongoni mwa wasanii wa kundi la RNE lenye maskani yake Hale Tanga, wako mbioni kuingia mkataba wa kutangaza Condom

Tshabalala aongeza miaka miwili Simba

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba SC, leo wamemuongezea mkataba wa miaka miwili beki wao wa kushoto Mohamed Hussein 'Tshabala' (21) na kumfanya asalie mpaka mwaka 2018. Tshabalala ameongeza mkataba huo wa miaka miwili hii leo katika ofisi za Rais wa Klabu hiyo Evans Elieza Aveva, kwa maana hiyo zile tetezi zilizokuwa zikivumishwa kwamba beki huyo ataelekea mitaa ya Jangwani sasa zimezimwa. Simba inaendelea kumalizana na nyota wake ambao mikataba yao inaelekea ukingoni, Nahodha wa timu hiyo Jonas Mkude naye anaweza kumalizana na uongozi wa Simba kama ilivyokuwa kwa Tshabalala