Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2016

JERRY MURO AIKINGIA KIFUA TFF

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MKUU wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga SC Jerry Cornely Murro amelikingia kifua Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF ambalo leo limemwandikia barua afike shaurini Jumamosi ijayo. TFF imemwandikia barua msemaji huyo wa Yanga kwamba ahudhurie ofisi za Shirikisho hilo Uwanja wa Karume Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazomkabili  Murro anadaiwa kutoa maneno ya kejeli kwa Shirikisho hilo. Lakini barua aliyotumiwa Murro haionyeshi kama anaitwa na kamati gani ya TFF zaidi ya kusema anaitwa na kamati, Naye Murro amesema hakubaliani na barua hiyo na yupo tayari kupambana na yeyote mwenye kutaka kumchafua yeye na Yanga

CHIRWA AIGAWA YANGA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM MSHAMBULIAJI mpya wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC Obrey Chirwa ameigawa timu hiyo hasa baada ya kucheza dakika 45 za mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Chirwa amecheza mchezo huo lakini ameshindwa kuwashawishi Wanayanga wote na kila mmoja anasema lake, mshambuliaji huyo raia wa Zambia aliyetua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea FC Platinum ya Zimbabwe alishindwa kuifungia Yanga bao wakati ilipolala 1-0 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Katibu wa Baraza la wazee la Yanga Ibrahim Akilimali alimponda nyota huyo kwa kushindwa kuonyesha cheche ikiwa amesajiliwa kwa pesa nyingi, lakini baadhi ya wanachama wa Yanga wakamshutumu mzee huyo wakidai mchezaji huyo bado anayo nafasi ya kung' ara

KOCHA MPYA SIMBA ATUA KUSAINI MKATABA

Picha
Na Prince Hoza KOCHA mpya wa klabu ya Simba Mcameroon Joseph Maurus Omog anatarajia kuwasili Alhamisi tayari kabisa kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo msimu ujao. Omog ambaye aliwahi kuzinoa Leopards ya DRC na Azam FC ya Tanzania zote akiziwezesha kupata ubingwa wa nchi, anataraji kuiongoza Simba kwa ajili ya msimu ujao na huenda akasaini mkataba wa miaka miwili. Habari ambazo Mambo Uwanjani inazo zinasema kuwa Omog atakuwa kocha mkuu ndiye atakayependekeza usajili wa wachezaji wa kimataifa, Omog alizaliwa Novemba 30, 1971 Cameroon na amekuwa kocha nwenye mafanikio. Msimu ujao Simba ishindwe yenyewe kutwaa ubingwa wa bara kutokana na bahati aliyokuwa nayo na uwezo pia, kikosi cha Simba kinasukwa upya huku Jackson Mayanja akitajwa kuwa msaidizi wake

RNE RAP NEWS YAWAPA MKATABA MNONO WASANII WA TANGA

Picha
Na Prince Hoza, TANGA KAMPUNI ya muziki ya RNE Rap News Intertainment yenye maskani yake jijini Tanga imeingia mkataba mnono na wasanii wa mkoani Tanga kwa lengo la kuwasaidia kimuziki ndani na nje ya nchi. Akizungumza na mtandao huu, mmoja wa wasanii wanaounda group la wasanii hao Mkola Man ambaye pia ni mwandishi wa michano amesema wamefurahia kuingia makubaliano na kampuni hiyo. "Nikweli tumesaini mkataba mpya chini ya RNE rap newz entertainment, itakayo simamia mambo yetu hususani muziki,  tunaamini MUNGU atatusimamia kufika mbali. kutokana na changamoto na ushindani uliopo kwenye gemu la sasa hivi. "Yussa Tyiger na Mkola Man tupo chini ya lebo hiyo. ambayo makampuni mbali mbali yamejitokeza kuisapoti nabado yanakaribishwa makampuni mengine na kuhusu lebo ya zamani jibu liko wazi asiye shukuru kido ndugu mwandishi awezi kushukuru kikubwa mchango wake ndugu Sakaingo bado upo kwenye kumbukumbu ya maisha yetu pia bila kuwasahau mashabiki wetu tunasamini mchango wao pia a...

YANGA WAJIFUA KINOMA ANTALYA

Picha
Na Ikram Khamees, ANTALYA MABINGWA wa soka Tanzania bara wanaendelea kujifua mjini hapa kujiandaa na mchezo wao wa kwanza kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya MO Bejaia ya Algeria. Yanga imeweka kambi yake katika jiji la Antalya ikifikia kwenye hoteli ya kifahali ya Rui, kocha mkuu wa mabingwa hao Mholanzi Hans Van der Pluijm amesema kambi yao ya Uturuki itawapa ushindi dhidi ya Waargeria hao. Kikosi hicho kinafanya mazoezi makali kuanzia asubuhi, jioni mpaka usiku na wachezaji wote wanaonekana kuwa ari, kasi na nguvu kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya mwalimu wao Hans na msaidizi wake Juma Mwambusi Mazoezi yanaendelea Hans Pluijm kazini Wachezaji wa Yanga wakipadha Wakipiga tizi muda wote

MAONI: SIMBA WEKENI MAMBO HADHARANI, USAJILI WA KIMYA KIMYA MAANA YAKE NINI

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM NIMEMSIKIA mwenyewe mwenyekiti wa kamati ya usajili klabu ya Simba Kapteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Zacharia Hanspoppe akisema kwamba Simba itafanya usajili wake kimya kimya. Maneno hayo si kwamba yamenikera mimi peke yangu hapana, wapo mashabiki wa Simba wameniandikia meseji kwamba hawafurahishwi na Hanspoppe  mashabiki hao wanataka bosi huyo wa usajili ajiweke kando ili awapishe wengine. Usajili wa kimya kwa sasa hauna maana yoyote ikiwa mchezo wa mpira unachezwa hadharani, hakuna faida yoyote ya kufanya usajili kwa kuogopa wenzako wanafanya nini. Hivyo namuomba Hanspoppe aachane na maneno hayo na awasajilie majembe Wanasimba ili wasuuzike na mioyo yao, Tetesi za usajili zimeanza kuenea kuwa Sinba wamemsajili kiungo wa Yanga Salum Telela. Mbali na Telela pia Simba inatajwa kukamilisha dili ya kumchukua mshambuliaji wa Ndanda FC ya Mtwara Atupele Green, Hanspoppe kutuambia usajili utakuwa wa kimya kimya anamaanisha nini! Paul ...

YANGA YATUA UTURUKI TAYARI KUWAVAA WAALGERIA

Picha
Na Ikram Khamees, Antaria, UTURUKI Mabingwa wa soka wa Tanzania bara Yanga SC wamewasili salama nchini Uturuki na wataendelea na mazoezi yao kwa ajili ya maandalizi yao ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga imefikia katika mji wa Antaria ambapo mazingira yake yanafanana kabisa na Algeria, mabingwa hao wa bara mara 26 watacheza na wenyeji wao MO Bejaia kabla hawaelekea Dar es Salaam kuwapokea TP Mazembe ya DRC. Ziara ya Uturuki itatumika kama sehemu ya maandalizi yao, Yanga imesafiri na wachezaji wake 21 huku wengine wakiachwa Dar es Salaam, mmoja kati ya wachezaji waliotua hapa Uturuki ni beki wa zamani wa Simba Hassan Kessy ambaye muda wote alionekana mwenye furaha

TELELA NJIA NYEUPE SIMBA

Picha
Na Salum Fikiri Jr, DAR ES SALAAM YANGA imeachana na mpango wa kumuongezea mkataba kiungo wake Salum Abdul Telela "Abo Master" na sasa njia nyeupe kwa mahasimu zao  Simba SC kunasa saini yake. Telela ambaye ameonyesha kiwango kikubwa kwenye kikosi hicho cha Yanga na kuisaidia kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo, Ligi kuu bara mara mbili mfululizo na kombe la FA, pia ameisaidia Yanga kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika. Mchezaji huyo mwenye nidhamu ya hali ya juu anatajwa kutemwa na kocha Hans Van der Pluijm ambaye hakuwa na maelewano naye mazuri, Simba walisikika wakimtaja kwenye usajili wao na sasa mambo yanaweza kuwa supa kwani Yanga wameshasitisha mpango wa kumpa mkataba mpya Salum Telela njia nyeupe kutua Simba

BEKI WA MTIBWA SUGAR AUAWA DAR

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM Matukio ya kinyama yanazidi kuongezeka kila kukicha hapa nchini na safari hii mchezaji wa zamani wa Toto Africans, Mtibwa Sugar, Azam FC na Vijana ya Ilala John Mabula amefariki dunia baada ya kuuawa kwa kuchomwa kisu. Kiungo wa zamani wa Yanga SC na Mlandege ya Zanzibar Deo Lucas ameitonya Mambo Uwanjani kuwa marehemu alikutwa na mauti akiwa na shemeji yake maeneo ya Kitunda Dar es Salaam. Deo anasema, Mabula akiwa anamsindikiza shemeji yake wakakuta kuna ugomvi njiani ambapo muda si mrefu wakavamiwa wote wawili yeye na shemeji yake na kushambuliwa na visu hadi kusababisha umauti. Mabula aliyetamba na kikosi cha Mtibwa kilichofanikiwa kuwa mabingwa wa bara mara mbili mfululizo 1999 na 2000 anatarajia kuzikwa Jumatatu jijini Dar es Salaam, kwa niaba ya mtandao huu unatoa pole kwa wafiwa na kulaani vikali vitendo vya mauaji ya kinyama John Mabula enzi za uhai wake

MICHANO: USTAADH JUMA NA MUSOMA, AMEISHIA KUJENGA NYUMBA KWA MATOFALI YA MABARAFU

Picha
Na Mkola Man, TANGA YAP.....yap....yap....Michano yangu ya leo inamchana Ustaadh Juma na Musoma aliyekuwa meneja wa kundi la muziki lijulikanalo kwa jina la Watanashati Family akiwamo PNC, Kitale, Dogo Janja na wengine. Hakika meneja huyu hakuwa nania ama malengo ya kweli kwa wasanii wake, alichokifanya ni kujenga nyumba kwa kutumia matofali ya mabarafu, akijuwa wazi jua likiwaka yatayeyuka. Hakuweka bajeti ya kutosha yenye lengo la mafanikio, kiukweli alikuwa anatafuta jina tu, mameneja kama hawa wapo wengi wameshindwa kupata mafanikio kwa mfumo wa mameneja feki kama wa Ustaadh Juma. Ila mwisho wa  siku lawama uwakumba wasanii  Michano inawachana mameneja wote feki, Tukutane wiki ijayo ni mimi Mkola Man........MwanaTanga

BEKI MPYA YANGA AULA CAF

Picha
Na Mrisho Hassan  DAR ES SALAAM BEKI mpya wa upande wa kushoto wa mabingwa wa Ligi kuu bara na kombe la FA, Yanga SC, Hassan Ramadhan Kessy ameula baada ya kocha mkuu wa mabingwa hao Mholanzi Hans Van der Pluijm kumwidhinisha katika usajili mpya CAF. Yanga inatakiwa kufanya usajili wa nyongeza hasa baada ya kufaulu kucheza hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika, kwa kufanikiwa hatua hiyo Shirikisho la soka Afrika CAF inazitaka timu zote zilizotinga hatua hiyo kusajili upya. Yanga sasa itasajili wachezaji wengine wawili au watano na tayari kocha wa mabingwa hao Hans Pluijm amependekeza majina ya nyota wawili wapya Hassan Kessy aliyesajiliwa kutoka Simba na Juma Mahadhi aliyetokea Coastal Union. Maana yake beii huyo na kiungo wa Coastal wameula kwani watacheza rasmi michuano ya CAF ambayo ni ya pili kwa ukubwa, Kessy akiwa na Simba hakuwahi kucheza michuano yoyote ya CAF hivyo ni sawa na kuangukiwa na bahati

MANJI ACHUKUA FOMU YANGA, AWAVUA UANACHAMA WALIOCHUKULIA FOMU TFF

Picha
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MWENYEKITI ya Yanga Yusuf Mehbood Manji leo ameamua kuchukua fomu ya kuwania tena nafasi yake ya uenyekiti katika makao makuu ya klabu hiyo Jangwani. Manji pia ametumia fulsa hiyo kuwavua uanachama wale waliokwenda kuchukulia fomu za kuwania uongozi makao makuu ya Shirikisho la mpira wa miguu TFF. Yanga leo imeanza mchakato wa kufanya uchaguzi wao mkuu unaotarajia kufanyika Juni 11, wakati ule uliohitishwa na TFF utafanyika Juni 25. Wakati huo huo Manji akitumia wadhifa wake amemvua uanachama aliyekuwa mwenyekiti wa matawi ya Yanga mkoani Dar es Salaam Mohamed Msumi na kuwasimamisha wengine wote waliodiriki kuchukulia fomu zao za kuwania uongozi TFF Manji akichukua fomu ya uenyekiti leo Manji akilipia ada yake ya uachama Manji akiwasili makao makuu ya klabu Jangwani Dar es Salaam Wanachama wa Yanga wakimshangilia Manji Umati ulijazana Jangwani kumshuhudia Manji aiichukua fomu Baadhi ya wapenzi wa Yanga wakipita na bango lao kumshutumu mw...

ANAYEKUMBUKWA: EMMANUEL GABRIEL MWAKYUSA YANGA HAWAKUPUMUA

Picha
Na Prince Hoza, DAR ES SALAAM MIAKA ya mwishoni na 90 na mwanzoni na 2000 alitokea mtu mmoja hatari sana Emmanuel Gabriel Mwakyusa aliyekuja kutikisa katika klabu ya Simba. Gabriel alitamba na klabu hiyo na akatokea kuwa mmoja kati ya qashambuliaji hatari kabisa kuwahi kutokea, pia akatamba na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars. Gabriel alisajiliwa na Simba sambamba na mshambuliaji mwenzake Godfrey Mhando lakini wakati huo Mhando alikuwa katika ubora wa hali ya juu. Alipotua Simba Gabriel alitokea kuwa shujaa na kumfunika kabisa Mhando waliotokea wote Nathareth ya Njombe, Gabriel alifanikiwa kutikisa kwa mabao yake na kuitungua Yanga mara tano. Watu wa Yanga wanamwogopa sana mshambuliaji huyo aliyepata pia kuzichezea Mtibwa Sugar, Prisons na Rayon FC ya Rwanda, Gabriel aliyezaliwa Mei 21, 1984, alikuwemo kwenye kikosi cha heshima cha Simba kilichoweka rekodi mwaka 2003. Simba mwaka huo iliingia hatua ya makundi Ligi ya mabingwa barani Afrika tena ikiitoa mashindanoni na kuivua...