RNE RAP NEWS YAWAPA MKATABA MNONO WASANII WA TANGA
Na Prince Hoza, TANGA
KAMPUNI ya muziki ya RNE Rap News Intertainment yenye maskani yake jijini Tanga imeingia mkataba mnono na wasanii wa mkoani Tanga kwa lengo la kuwasaidia kimuziki ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na mtandao huu, mmoja wa wasanii wanaounda group la wasanii hao Mkola Man ambaye pia ni mwandishi wa michano amesema wamefurahia kuingia makubaliano na kampuni hiyo.
"Nikweli tumesaini mkataba mpya chini ya RNE rap newz entertainment, itakayo simamia mambo yetu hususani muziki, tunaamini MUNGU atatusimamia kufika mbali. kutokana na changamoto na ushindani uliopo kwenye gemu la sasa hivi.
"Yussa Tyiger na Mkola Man tupo chini ya lebo hiyo. ambayo makampuni mbali mbali yamejitokeza kuisapoti nabado yanakaribishwa makampuni mengine na kuhusu lebo ya zamani jibu liko wazi asiye shukuru kido ndugu mwandishi awezi kushukuru kikubwa mchango wake ndugu Sakaingo bado upo kwenye kumbukumbu ya maisha yetu pia bila kuwasahau mashabiki wetu tunasamini mchango wao pia atuwezi kuhusahau mchango wa Dr Mlipu Pamoja na wadau wote", alisema